Muda Ni Maisha


Nakumbuka kipindi Nipo shule, ( High level) kuna mwalimu nilikuwa namchukia sana kwa sababu alikuwa makini na MUDA, Asubuhi MUDA wa Mchaka Mchaka ilikuwa ni lazima ukimbie, na muda wa darasani ni lazima uwepo na asikuone nje unazurura, Hali hii ilimpelekea achukiwe na wanafunzi wengi ikiwemo mimi, lakini mwisho wa yote alikuwa ametusaidia pakubwa sana kufikia MALENGO yetu kiafya, kinidhamu na kitaaluma kwa kuzingatia muda.

MUDA ni kipindi au kipimo cha wakati ambacho hutumika kufanya shughuli au matukio mbalimbali.

👉Ni rasilimali muhimu ambayo haiwezi kurudishwa nyuma baada ya kutumiwa. Muda unaweza kugawanywa katika vipindi vya sekunde, dakika, saa, siku, miezi, au hata miaka. Kwa kifupi, muda ni kipengele muhimu katika maisha yetu ambacho kinaathiri jinsi tunavyoishi na kufanya maamuzi.
JE, NAWEZAJE KUSIMAMIA MUDA WANGU VIZURI?
Leo hii, si ajabu kumkuta mtu amekaa sehemu ukimuuliza unafanya nini? anakwambia Nipo tu napoteza muda hapa. Lakini wakati huohuo, kuna mtu mwingine hata ukimpigia simu anakwambia nitafute badae niko bize sana.

Hapa nataka tuone namna Gani tunaweza kusimamia muda wetu vizuri.
👉 Kupanga Ratiba, haijalishi upo Katika hali gani, Kupanga Ratiba ni kitu Cha muhimu sana, Inashangaza kumuona mtu leo hii anaamka na hajui anakwenda kufanya nini kazini au hata mahali popote. Mtu huyu Huwa anafanya vitu bila mipango, atafanya hiko ataacha, atafanya kile ataacha, Musa utaisha na hajakamilisha hata kitu cha maana.

👉Kutambua vipaumbele, Vile vitu vya muhimu zaidi vinapaswa kupewa kipaumbele kisha vingine vinafuata. Hali hii inapelekea kutunza mudavizuri. Mfano, upo kazini, ghafla Kuna mgeni amekuja na haikuwa na miadi nae, hautapata dhambi ukimwambia akusubiri umalizie shughuli zako kisha uonane nae.

👉Kujifunza kusema hapana. Sio kila jambo ulichukue, mengine yanakupotezea muda hivyo tujifunze kusema hapana kwa Yale mambo ambayo hayana umuhimu.

👉Mapumziko. Hakikisha unajipa Mapumziko ili kupumzisha mwili. Usifanye Kazi muda wote, akili itachoka utashindwa kuendelea Kufanya Kazi nyingine kwa wakati sahihi.

Makala hii imeandikwa nami,
Latifa Omary Sharifu
0718402449
Morogoro_ Tanzania


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X