Ninahitaji Watu Watano, Nami Nitawasaidia Kuandika Na Kukamilisha Kitabu Ndani Ya Miezi Mitatu Mpaka Sita


Ninahitaji Watu Watano, Nami Nitawasaidia Kuandika Na Kukamilisha Kitabu Ndani Ya Miezi Mitatu Mpaka Sita

Rafiki yangu mpendwa habari ya leo.

Kwa siku sasa nimekuwa nikiwasaidia watu mbalimbali kuandika vitabu vyao. Watu ambao tokea mwanzo walikuwa hawafikirii kama wanaweza kuandika vitabu vyao, nimewasaidia kuweza kuandika na kukamilisha vitabu vyao.

Katika uandishi wa vitabu huwa nafanya watu katika ngazi kubwa tatu.

Ngazi ya kwanza, nakupa mwongozo, unapambana unaandika mwenyewe kitabu.

Ngazi ya pili, tunaandika kwa pamoja. Unaandika, unaleta kazi yako kwangu, naipitia, nakupa mrejesho wa kitalaam.  Kisha unaendelea kuboresha kazi, mpaka pale tunapokuwa tumeweza kupata kazi ambayo ni bora kabisa. Mwisho kazi inakuwa ya kwako.

Na kwenye ngazi ya tatu, nimekuwa ni mimi kukuandikia kitabu chako moja kwa moja. Na hapa zaidi nimekuwa nawasaidia wale ambao wanaandika historia za maisha yao au wapendwa wao (autobiography)

Wengi niliowasiaidia kuandika historia za maisha yao au wapendwa wao,  wao wa karibu wamefurahia sana hizi huduma.

Kuna wengine wamekuwa wanapenda kupata hizi huduma, ila changamoto yao kubwa wamekuwa wakiniambia kuwa gharama ni kubwa.

Sasa leo nina habari njema kwa ajili yako.

Naam, nina habari njema mno.

Ili unielewe vizuri iko hivi.

Kwa wale ambao nimekuwa nawapa mwongozo na wanaandika wenyewe mwanzo mpaka mwisho, gharama yake imekuwa ni shilingi 50,000/-

Kwa wale ambao wamekuwa wanashiriki program ya uandishi kwenye ngazi ya pili, yaani, kuandika pamoja nami, basi wamekuwa wanalipia kati 250, 000 mpaka milioni moja kulingana na aina ya kitabu husika.

Na kwa waleo ambao nimekuwa nawaandikia, wamekuwa wanalipia milioni tano (5,000,000)! Ambapo nimekuwa nawaandikia kitabu mwanzo mpaka mwisho.

Sasa leo nina habari njema kwa ajili yako wewe.

Kama ungependa kuandika kitabu chako, USHINDWE WEWE MWENYEWE TU! Ndio, ushindwe mwenyewe.

Kumbuka hizi gharama utakazoona hapa ni kwa ofay a watu watano tu. Gharama zitakuwa hivi. SOMA VIZURI MAELEKEZO NA UCHUKUE HATUA SAHIHI.

Kama utataka nikupe mwongozo na uandike wenyewe mwanzo mpaka mwisho, gharama yake itakuwa 30,000/-

Kama utashiriki kwenye hii program ya uandishi kwenye ngazi ya pili, yaani, kuandika pamoja nami, basi Utalipia shilingi 150,000/- na utaruhusiwa kulipia 50,000/- kila mwezi kwa kipindi cha miezi mitatu ambacho tutakuwa tunafanya kazi pamoja. Kama kazi itazidi miezi mitatu, utaendelea kulipia 50,000 kila mwezi mpaka tutakapomaliza.

Kama utataka nikuandikie kitabu mwenyewe, utalipia milioni moja na nusu. Utalipia kiwango cha 250,000 kila mwezi kwa kipindi cha miezi sita.

Kwa nafasi za kuandikiwa kabisa sasa hivi nina nafasi mbili tu KWA SASA. Maana siwezi kwenda na watu wengi kwa wakati mmoja.

Kama utachangamka sasa. Tutaanza kazi.

NB: hii haitahusisha gharama za usafiri na malazi pale nitakapohitajika kusafiri na kufika eneo walipo wahusika ambao nitafanya nao mahojiano.

Kama upo tayari, nicheki, sasa tufanye jambo.

Tumia namba ya simu 0755848391 au wasiliana na msaidizi wangu kwa 0655 848 392

Email: songambele.smb@gmail.com

SOMA ZAIDI: KAMA UNAFIKIRI KILA KITU KILISHAANDIKWA, FIKIRI TENA (SABABU 18 Kwa Nini Tunaandika Vitabu na Tutaendelea Kuandika Vitabu, Na Kwa Nini Wewe Unapaswa Kuandika Cha Kwako)


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X