UTANGULIZI
1. Mwandishi wakitabu hiki anatujuza kwamba maisha tunao ni nishati yani kila tofali(seli ) mwilini ni nishati kutokana na fomula ya Albert Einstein:
E=MC2 E= Nishati, M= mwili C = kasi ya mwanga
Kwa hivyo basi, tunao uwezo mkubwa hapa duniani kiasi kwamba huwa tunazo nguvu zakufanya chochote kile tutachodhamiria kufanya, ubunifu, kuyafanya makubwa yoyote tutakapowaza ili kuipanua na kuigeuza dunia kwa mafanikio makubwa kwa makusudi yetu binadamu.
2. Matokeo makubwa huwa yaweza kufanyika pale tutageuza fikra zetu kiakili na mwisho wa siku maisha yetu vile itakuwa nzuri mno.
3. Mhimu zaidi kwanza tunapaswa kuwa na mawazo na mipango mikubwa ya picha au ramani ya maono tunao ya kile tunachopenda au tunachotaragia kutokea kwa uhalisia hapa duniani na kukifanyia kazi.
4. Ramani hii hapa ya maono yako ya siku za mbeleni, huwa itakutia hamasa kubwa ya kujishangilia , na kuwa msukumo wako wa kufanya kile unachotaka kutokea bila kuacha na maro zote kuwa makini bila kutoka kwenye mstari.
5. Mwandishi huyu anachosisitiza kwa nguvu sana ni kuyafanya malengo yako kwanzia na lengo moja likamilishe kisha fanya lingine ukitumia upendo, uvumilivu na unyenyekevu wako wote wakati unapotenda kazi yako kuhusu lengo husika.
Aidha anatukumbusha kwamba dunia nzima inakusubiri na kukusikiliza mpaka pale utayatimiza maono yako!
Yupo tayari?
Mwandishi Dr Busingye Warugaba Amos
Mkurugenzi mku wa WARUGABA AMOS MEDICAL CENTER
mawasiliano kwa:
Simu: 256772367793/ 256708470471
Barua pepe: amosbusingye05@gmail.com
Tovuti: https://warugabamedicalcenter.com