Tuna mengi ya kujifunza kutoka kwa wachina. Ni Pipi china, kuliko kuinunua kwa Mangi Mtaani Kwako!


Siku siyo nyingi nilikuwa nikitafuta kipaza sauti cha kutumia kwa ajili ya kazi zangu. nilijaribu kuangaza hapa na pale kwa wasambazaji wa hivi vifaa hapa tanzania, ila kwa bahati mbaya sikufanikiwa.

Hivyo, ilinibidi niagieze hivi vifaa kwa njia ya mtandao. Ilibidi niagize hivi vifaa moja kwa moja kutoka china.

Kitu cha kwanza nilichokutana nacho ni kwamba hivi vifaa vilikuw ani bei ndogo china. Hili halishangazi sana kwa sababu tunajua wazi kuwa asilimia kubwa ya bidhaa zinazouzwa hapa nchini zinaagizwa chini.

Lakini kitu kingine ilikuwa ni kwamba hizo bidhaa zilikuwa zinakuja bure mpaka hapa Tanzania. Hiki kitu kilikuwa kama masihala vile, lakini cha kushagaza ni kwamba, mizigo hiyo niliyoagiza, imekuja bure kabisa mpaka inanifikia.

Gharama ya ziada niliyolipa ni buku (elfu moja ya boda) ILI KUUFIKISHA MZOGO OFISINI kwangu.

Zaidi ya hapo hakukuwa na gharama nyingine ya ziada. Nilinunua hizi

Makala ya leo nimeona nieleze hili.

Tuna mengi ya kujifunza kwa wachina, na hili nalo ni jambo la kujifunza kutoka kwao.

Wanawezaje kusafirisha mzigo wa 12 kutoka china mpaka Morogoro nchini Tanzania bila kuniambia niongeze gharama za ziada.

Ebu tuongee kibongobongo kwanza.

Ebu pata picha uko zako Kamachumu-Muleba-Kagera nchini Tanzania.

Au Zako Mvuha, morogoro vijijini, Morogoro.

Unaagiza mzigo wako Kariakoo, Gharama za kupokea mzigo kwneye maeneo hayo zinaweza kuwa ni kubwa ya gharama za kununulia mzigo husika.

Hata mimi niliye Morogoro mjini bado mfano gharama ya mzigo wa elfu tano kunifikia ni kubwa kuliko gharama ya kununulia mzigo wenye thamani hiyo ya elfu tano.

Kwenye hili tujifunze kwa wachina, namna wanavyofanya, kisha tuone namna ya kuboresha.

Nasema hivi kwa sababu mimi mwenyewe ni mmoja wa watu ambao huwa wanatuma sana vitabu.

Zamani nilikuwa naweza kutuma kitabu kimoja kwa shilingi elfu tano tu.

Ila leo hii bila ya kuwa na shilingi elfu kumi, siwezi kutuma hata bahasha. Labda kama natuma mzigo kutoka hapa Morogoro kwenda Dar au Dodoma na muda mwingine Arusha na Kilimanjaro.

Nje na hapo, napaswa kuwa na noti ya msimbazi.

Unadhani ni mambo gani zaidi tunahitaji kuendelea kujifunza kutoka kwa wachina

Tunahitaji tujifunze na tuanze kufanyia kazi, haya tutakayojifunza kutoka kwa wachina.

Unajua kwa nini?

Kwa sababu, wachina wao pia wamekuwa wanajifunza na kuiga sehemu nyingine na kufanyia kazi yale wanayojifunza haraka.

Tusipochangamka, mimi nakwambia miaka mitano ijayo. Itakuwa ni bora kuagiza mzigo china, kuliko kwenda kununua kwa mangi hapo mtaani kwako.

Tujifunze, tuchukue hatua, la sivyo biashara nyingi siku zijazo zitakuwa hatarini.

Imeandikwa nami

Godius Rweyongeza

0755 848 391

Morogoro-Tz


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X