Una mpango wa kujiajiri? Hakikisha kuwa hauchukui hatua ya kujiajiri kama huna ufahamu wa jambo hili Moja.
Jambo hili ni kwamba, kama huwezi kujisimamia mwe yewe kutekeleza majukumu Yako, usijiajiri.
Kama Bado unasubiri watu wakusimamie ndiyo utekeleze majukumu Yako, usianzishe biashara ya namna yoyote.
Pengine unajiukiza Kwa Nini.
Jibu la haraka ni Kwa sababu hiyo biashara Yako itakufa.
Jibu refu
Ni kwamba kama unaanzisha biashara na uko pekee Yako maana yake hakutakuwa na mtu wa kukusimamia. Mtu ambaye atakufuatilia mwenendo wako wote hatua Kwa hatua, kujua kama umefanya na kukamilisha majukumu husika au hujafanya.
Sasa kwa kuwa mtu wana mna hii atakuwa hayupo, na wewe mara zote huwa unategemea kusimamiwa.
Nakuhakikishia kwamba itakuwa vigumu sana kwako kufika mbali.
Kitu cha kipekee ambacho unahitaji ni uwezo wa wewe kujisimamia. kujisimamia kwenye kufanya kazi na majukumu mengine
Kama huwezi kufanikisha hili, basi hata usithubutu kujiajiri. Huo ndio wosia wangu kwako.