Rafiki yangu mpendwa salaam, utajiri ni haki yako ya msingi ambayo unapaswa kupata. Tofauti kubwa ya haki hii na nyingine ni kwamba unapaswa kuipambania.
Wakati haki nyingine zinadaiwa mahakamani, utajiri haudaiwi mahakamani. Utajiri unakuja kwa kutokwa na jasho, damu na machozi.