Aina Tano Za Uwekezaji Ambazo Unaweza Kufanya Leo Hii, Zikakupa Faida Hapa Duniani Na Hata Pale Uakapokuwa Umetangulia Ahera


Kuna aina za uwekezaji ambazo unaweza kufanya leo hii, zikaweza kukuletea faida ukiwa hapa duniani, hata itakapofika hatua ukatangulia mbele ya haki, bado utakuwa unaengeneza faida hapa duniani. Unajua aina hizi za uwekezaji ni zipi?

 

Aina ya kwanza ni uwekezaji kwenye hisa

Kama utachagua aina nzuri ya uwekezaji na ukaufanya kwa msimamo, nakuhakikishia kuwa utatengeneza faida ukiwa hapa duniani, na uaengeneza faida ukiwa ahera. Kiufupi ni kwamba wale watu utakaokuwa umewaacha, wataendelea kupata gawio kwa siku nyingi sana hata baada yaw ewe kuwa umetoka hapa duniani.

Uwekezaji kwenye hisa ni njia nzuri ya kutengeneza faida ukiwa hapa duniani. Unapowekeza katika hisa za kampuni ambazo zina faida, unaweza kupata gawio la faida na pia thamani ya hisa zako inaweza kuongezeka kwa muda. Hata baada ya wewe kufariki, wale walioachiwa urithi wako wanaweza kuendelea kupata gawio na faida kutokana na uwekezaji huu.

 

 

Aina ya pili ni uwekezaji kwenye vipande.

Vipande au mutual funds ni njia nyingine bora ya uwekezaji. Kwa kuwekeza kwenye vipande, unakuwa unachangia kwenye mfuko ambao unawekeza kwenye hisa na dhamana mbalimbali. Hii ni njia nzuri ya kupunguza hatari na kuongeza faida. Faida zinazopatikana zinaweza kuendelea hata baada ya kifo chako, na hivyo kuwanufaisha warithi wako.

Kama ulivyo uwekezaji kwenye hisa. Uwekezaji kwenye vipande na hasa utt amis, ni sehemu nzuri sana ambayo itakuwezesha kuengeneza faida hapa duniani. Na haa baada ya  ya wewe kuwa umeaga dunia, wau utakaowaacha hapa duniani, wataendelea kuengeneza faida kwa siku nyingi zitakazofuata.

 

Aina ya tatu ni uwekezaji kwenye hatifungani.

Na hasa hatifungani za serikali. UNAJUA KWA NINI? KWA sababu ni ukweli kuwa serikali haiwezi kuffilisika na hata kuacha kuwalipa wananchi wake. Hivyo, ukiwekeza kwenye hatifungani za serikali maana yake utaweza kupata  faida ukiwa bado hapa duniani, lakini habari njema zaidi ni kwamba, kama utaaga dunia, basi uwekezaji wako bado utaendelea kuwanufaisha wale autakaokuwa umewaacha.

Aina ya nne ni ya uwekezaji ni uandishi wa kitabu. Kitabu ni kitu kingine ambacho kama utakifanya, kitakufanya upate faida hapa duniani, lakini pia hata baada ya kuwa umetoka hapa duniani, bado utaendelea kuengeneza faida zaidi.

Kuandika na kuchapisha vitabu ni uwekezaji wa kipekee. Vitabu vinaweza kuuza kwa muda mrefu na kuleta mapato kupitia mauzo na mirabaha. Ikiwa kitabu chako kitakuwa maarufu, kitaleta faida kwa muda mrefu, hata baada ya wewe kufariki, na faida hizi zinaweza kuendeleza familia yako au mirathi yako.

 

Aina ya tano ni uwekekezaji kwenye katika Mali Isiyohamishika

Kununua ardhi au majengo ni uwekezaji thabiti ambao una faida ya muda mrefu. Thamani ya mali isiyohamishika kawaida huongezeka kwa muda, na unaweza kupata mapato ya kodi kama ukiamua kupangisha. Hata baada ya wewe kuondoka duniani, mali hizi zinaweza kuendelea kuleta faida kwa warithi wako.

Aina ya sita ni Uwekezaji katika Biashara

Kuanzisha na kuendesha biashara yenye faida ni njia nzuri ya kutengeneza kipato kikubwa. Biashara inaweza kuendelea kuendeshwa na warithi wako na kuleta faida kwa muda mrefu hata baada ya wewe kufariki. Kumbuka hapa biashara ninayoongelea siyo hizi biashara nyingi ambazo zimekuwa zinafanywa kwa mazoea na watanzania walio wengi. Bali ni biashara ambazo zinajiendesha zenyewe kwa faida kubwa.

Aina ya saba ni uwekezaji kwenye elimu ya watoto.

Kwa kuwa watoto wako ndiyo watakuwa wanaendesha hivi vitu na wanapaswa kuendelea kuviendesha kwa siku nyingi zinazokuja, basi unapaswa unapaswa kuwajengea msingi mzuri wa kujifunza  na kuwap elimu sahihi. Ili kazi yako kubwa isiishie tu kwenye kuanzisha hivi vitu, bali watoto wako waweze kuendelea kuendesha hivi vitu kwa siku nyingi zinazokuja.  Hivyo wajengee sehemu sahihi.

 

Hizi aina za uwekezaji ni uhakika, zitakupa faida ukiwa hapa duniani na hata baada ya kuwa umeaga dunia. Kwa kuchagua uwekezaji mzuri na kwa kufanya maamuzi ya busara, unaweza kuhakikisha kuwa una faida hapa duniani na pia baada ya kuondoka duniani, wale unaowaacha wanaweza kufaidika kwa muda mrefu pia.

Makala hii imeandikwa n Godius Rweyongeza

Kujifunza zaidi kuhusiana na aina hizi mada ambazo nimeeleza hapa. Hakikisha unapata nakala mbil za vitabu. Kwanza ni kitabu cha maajabu ya kuwekeza kwenye hisa, hatifungani na vipande pamoja na kitabu cha Jinsi ya kuw amwandishi mbobevu.

Kupata nakala yako ni rahisi sana. Lipia 25,000 ambayo ni gharama ya kila nakala. Tuma kwa 0684 408 755 ili uweze kutumiwa nakala yako. Baada ya kufanya malipo, tafadhali wasiliana na namba hiyo hiyo kwa ajili kufanya utaratibu wa kutumiwa vitabu vyako.

 

 


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X