MAMBO 6 YA KUACHA ILI UFANIKIWE


MAMBO 6 YA KUACHA ILI UFANIKIWE
Ili uweze kufikia Malengo na MAFANIKIO unayotaka lazima ukubali kuacha baadhi ya mambo
🤷MAFANIKIO kwako yanaweza kuwa na maana tofauti ,Kila mmoja wetu na wengi wetu hutafsiri MAFANIKIO ni kama Pesa,umaarufu,majumba,magari,.Wengine hutafsiri kama MAFANIKIO kwako ni furaha,Amani,uhuru,inategemea ni JINSI Gani unaweza kutafsiri MAFANIKIO kwako wewe mwenyewe

👉Ukijua maana ya MAFANIKIO kwako basi ni MUHIMU sana kujua mambo ambayo yanaweza kukuzuia wewe KUFIKIA MAFANIKIO katika MAISHA
👇👇
1)ACHA KUTAFUTA NJIA FUPI ILI KUFANIKIWA
-Itakuwa mbaya sana kama utafanya hivyo MAFANIKIO ya kweli katika chochote unachotaka utafanikiwa kwa kufanya kazi kwa bidii


2)ACHA KUWA NA MAWAZO MGANDO
-Uwezo au ujuzi wa mtu unatakiwa uwe na MAWAZO ya kukua na aina hii ya MAWAZO utafanya kazi kuwa vizuri zaidi na kupata uzoefu zaidi
3)ACHA KULAUMU WENGINE
-Utakapofeli katika jambo lako acha KULAUMU wengine siku zote kubaki kuwa wewe mwenyewe ndie unaehusika kwa kiasi kikubwa


4)ACHA KUSEMA SINA MUDA
_Anza kuanza kutumia muda wako vizuri na uache kusema huna Muda mwingine wa kufanya jambo la ziada
Tuna muda wa kiwango sawa kama wengine kwa siku ni kuamua ni njia gani utakavyo tumia Muda wako

5)ACHA KUTEGEMEA KUPATA ZAIDI BILA YA KUFANYA ZAIDI
-Unatakiwa kufanya kazi kwa bidii Ili kupata promotion au mshahara mkubwa kazini biashara zilizofanikiwa kupata mapato mengi kwa kutoa THAMANI kwanza kwa WATEJA wao na kupata MAFANIKIO. Acha kusubiri Mpaka mambo yakae sawa ndio uanze kufanya kazi kwa bidii

6)Acha kusubiri
-Usikubali uoga wako ukurudishe nyuma chochote ulichokuwa unapanga, unaota,unawaza kama ulipanga kuanzisha biashara chukua hatua hiyo sasa weka uoga pembeni na Anza kufanya kitu

Makala hii imeandaliwa nami,
Faith Mark Mrema
0742 825 286
Tanzania_Morogoro


One response to “MAMBO 6 YA KUACHA ILI UFANIKIWE”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X