Muda wa kuandika Kitabu unausubiri utoke wapi?


Utasikia mtu anakwambia nasubiri siku niwe na muda wa kutosha Ili niandike.

Sikiliza. Tena sikiliza vizuri. Muda wa kutosha haupo.
Hakuna mwandishi mwenye muda wa kutosha.
Kila mwandishi yuko bize.

Ila muda mchache TU anaopata anaandika. Hata wewe Fanya hivyo.

Kusubiri muda wa kutosha Ili uandike kitabu chako ni uongo. Hatusubiri tuwe na muda wa kutosha Ili tule, hatusubiri tuwe na muda wa kutosha Ili tuonge. Hata kama tuko bize, tutatafuta muda TU Ili tule na kuoga

Sasa inakuwaje tunasubiri muda wa kutosha Ili TUANDIKE? Tunasubiri muda huu utoke wapi?

www.songambele.co.tz


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X