Siku za nyuma nimewahi kuandika nakala inayoeleza sababu 18 Kwa Nini tunaandika vitabu na Kwa Nini wewe unapaswa kuandika Cha kwako.
Unaweza kupata na KUSOMA makala hii hapa
Au unaweza kuisikiliza pia Kwa sauti hapa
Sasa mbali na hizo sababu hapo juu. Kuna ndugu anataka kujua sababu za kiuchumi TU ambazo ndizo ziwe chachu ya kumsukuma kuandika.
Mara Kwa mara nimekuwa nikiwaambia watu kuwa kama sababu pekee ya wewe kuandika Kitabu Chako ni PESA. Bora usiandike kitabu chako
Kwa sababu utakata Tamaa. Na hiki kitu kimewatokea waandishi Wengi sana.
Unakuta mtu anaandika kitabu, lakini kuuza hata nakala 50 TU ni changamoto.
Kwa nini
Naomba unisikilize vizuri Sasa
Kwa sababu usomaji wa vitabu nchini Tanzania Bado upo chini ukilinganisha na nchi nyingine na hasa nchi za Ulaya. Kwa hiyo, kuuza vitabu kunahitaji usiwe TU mtu ambaye anataka PESA pekee Bali mtu ambaye upo tayari kuona watu wanapata mabadiliko kupitia maandishi Yako.
Kutakuhitaji kujitoa.
Kutoa elimu Kwa watu.
Hivyo Unapoandika Kitabu unapaswa kuwa na msukumo zaidi ya kutengeneza Fedha. Na hasa msukumo wa kuwasaidia watu waweze kuboresha maisha Yao.
Hili kitakupa NGUVU zaidi na hata ikitokea mauzo ya vitabu hayaendi vizuri Bado utakuwa una msukumo mkubwa Kwa sababu unajua ujumbe wako ulio kitabu ni, ukileta matokeo chanya Kwa mtu mmoja, unakuwa umeweza kufanya mchango mkubwa Kwa jamii.
Ni Nini msukumo wako wa kuandika Kitabu?
Karibu SONGAMBELE CONSULTANTS
✅ Tunakuandikia kitabu chako (ghostwriting)
✅ Tunatoa mwongozo wa kuandika kitabu chako
✅ Kuhariri vitabu
✅ Tunatoa usimamizi wa karibu kwenye uandishi wa kitabu chako
✅ Tuna vitabu bora vyenye hatua muhimu za kufuata katika uandishi
✅Na hata kuchapa kitabu chako
Mawasiliano:
Simu/WhatsApp: +255755848391
Email: jifunzeuandishi@gmail.com
Eneo: Morogoro mjini; Mafiga, Tenki Bovu
Telegram: https://t.me/jifunzeuandishi