Watu wengi huwa wakifikiria kuhusu kuandika kitabu, basi kitu cha kwanza ambacho huwa kinakuja kwenye akili yao ni kwamba unapaswa kuwa mtu wa pekee kabisa.
Nakubaliana na watu hawa kwamba ili kuandika kitabu chako unapaswa kuwa wa pekee. Na upekee mkubwa ambao unauhitaji wewe ili kuandika kitabu chako na kukikamilisha ni NIDHAMU YA KUKAA CHINI NA KUANDIKA.
Ukweli ni kuwa bila ya kuwa na nidhamu hii, hata kama utautaka uandishi kiasi gani, huu uandishi hautakuja kwenye uhalisia, hata kama utakuw ana wazo zuri kiasi gani la kuandika. Wazo hili halitakuja kwenye uhalisia kwa sababu hujakaa chini na kuandika. Hivyo, kama unataka unataka kuandika vitabu KAA CHINI ANDIKA.
Hiki ni kitu pekee unachohitaji.