Rafiki yangu wa ukweli, salaam. Hongera sana kwa siku hii nyingine ya kipekee sana. Leo ikiwa ni tarehe 30/7/2024, ni siku nyingine ambayo unapaswa kwenda kupambana.
Siku ya leo, nimeona nikwambie vitu vidogo ambavyo watu wanapuuza, ila mwisho wa siku vinakuwa na madhara makubwa.Ndiyo, ni vitu vidogo, lakini ukivipuuza, madhara yake yanakuwa ni makubwa sana.
Kitu cha kwanza ni muda. Sote tayari tunajua umuhimu wa muda kwenye maisha ya kila siku. Lakini ni wachache sana ambao huwa wanaheshimu muda. Muda ni rasilimali ambayo ukiipoteza hutaipata tena.
Kitu cha pili. Ni kutokuwa na msimamo kwenye vitu wanavyofanya. Kukosa msimamo kwenye kazi unazofanya, au kufanya leo na kesho ukaacha, kitu hiki kinapelekea wewe kukosa mwendelezo kwenye kile unachofanya.
Tatu ni kutaka mafanikio ya haraka, hiki ni kitu kingine ambacho kinawaangusha wengi. Unachotakiwa kufanya ni kuhakikisha unakuwa kwenye mchakato kwa muda mrefu. Ukikaa kwenye mchakato, bila kuhitaji kupata mafanikio ya haraka, basi hili litakusaidia wewe kuweza kufika mbali.
Nakutakia kila la kheri.
Karibu sana