Kama kuna mtu ambaye unaona kwamba ameweza kufikia mafanikio makubwa, basi ujue kwamba kuna gharama ambazo ameliipa na wewe hujalipa hizo gharama, unapaswa kuwa tayari kulipa gharama ambazo mtu huyu amelipa ili uweze kufikia kwenye ngazi ambazo yeye amefikia.
Kama unataka kujenga biashara kubwa ambayo itakufikisha kwenye ngazi ya ubilionea unapaswa kuwa tayari kulipa gharama ambayo itakufikisha kwenye hicho unachotaka kufanya.
Upo tayari kulipa gharama. Kama haupo tayari kulipa gharamam usitegemee kupata matokeo makubwa.
Wahenga wanasema kwamba ukitaka cha uvunguni ni sharti ukubali kuinama kwanza.
Hii ndiyo kusema kwamba ukitaka kula vinono, unapaswa kuwa tayari kuumia kidogo. Unapaswa kuwa tayari kulipa gharama ya kupata hivyo vinono ndiyo uje kuvipata.
Nakutakia siku njema rafiki yangu.
Kwenye kitabu cha JINSI YA KUFIKIAI NDOTO ZAKO; Nimeeleza gharama tano ambazo unapaswa kulipa. Na gharama hizi ni….au basi, pata nakala ya kitabu hiki ili uweze kusoma na kuzijua gharama hizi. Kupata nakala yako, tuwasiliane kwa 0684408755 sasa ili uweze kujipatia nakala yako.