Unakuwa na vitu Gani vingi vinavyokunya ukose hata dakika 15 za Kuandika kila siku?
Kuandika kunahitaji nidhamu. Kama ambavyo kusoma darasani kunahitaji nidhamu ili ufaulu, Kuandika pia kunahitaji nidhamu. Nidhamu ya Kuandika. Ukiona mtu ameandika na kitabu chake kimekamilika, ujue Moja ya gharama aliyoilipa ni nidhamu ya kukaa chini na Kuandika.
Kuandika hata pale alipokuwa hajisikii Kuandika.
Kuandika hata pale alipoona kama vile kaishiwa na mawazo ya Kuandika.
Kuandika hata pale alipokuwa amezungukwa na vishawishi vingi vya kumfanya asiandike.
Unapaswa kuwa na hii nidhamu, la sivyo unaweza kukuchukua Miaka mingi unaendelea tu kutamani Kuandika ila hujawahi Kuandika.
Siku ya leo, sahau yote, Tenga dakika 15 tu. Kaa chini andika
Ukikwama uliza. Nitakusaidia.
Kila la kheri