Notice: Function _load_textdomain_just_in_time was called incorrectly. Translation loading for the uncanny-automator domain was triggered too early. This is usually an indicator for some code in the plugin or theme running too early. Translations should be loaded at the init action or later. Please see Debugging in WordPress for more information. (This message was added in version 6.7.0.) in /home/songambele/public_html/wp-includes/functions.php on line 6121

Notice: Function _load_textdomain_just_in_time was called incorrectly. Translation loading for the health-check domain was triggered too early. This is usually an indicator for some code in the plugin or theme running too early. Translations should be loaded at the init action or later. Please see Debugging in WordPress for more information. (This message was added in version 6.7.0.) in /home/songambele/public_html/wp-includes/functions.php on line 6121
Maisha ni wajibu wako, ukishinda ni juu yako, ukishindwa ni juu yako pia - SONGA MBELE

Maisha ni wajibu wako, ukishinda ni juu yako, ukishindwa ni juu yako pia


Usije ukafanya kosa la kutaka kuwaachia wengine jukumu la maisha yako. Hakuna mtu anayeweza kujali kuhusu maisha yako kama wewe mwenyewe. Wewe ndiye mtu wa kwanza unayepaswa kujali kuhusu maisha yako kabla ya mtu mwingine yeyote.
Na unapaswa kulifanyia kazi kwa uhakika bila ya kurudi nyuma wala kukubali kukwamishwa na mtu au kitu chochote.
Kuwa na ndoto kubwa. Lakini ndoto hizi usiishie tu, kuwa nazo bila kuzifanyia kazi. Ukweli ni kuwa hakuna mjomba, shangazi au mama mdogo ambaye atafanyia kazi malengo na ndoto zako kubwa ulizonazo. Ni au uzifanyie kazi wewe mwenyewe au la uachane nazo kabisa.
Hilo ni jukumu lako, ndiyo maana nasema kwamba maisha ni wajibu wako, ukishinda ni juu yako mwenyewe na ukishindwa ni juu yako mwenyewe.

Kwa kuwa wewe umeamua kubeba jukumu la maisha yako, leo hii. Hakikisha Unasoma kitabu cha JINSI YA KUFIKIA NDOTO ZAKO. Kitabu hiki kinakueleza ukweli mmoja tu kuwa, usipofanyia kazi malengo nandoto zako, kuna mtu atakuajiri, kufanyia kazi malengo na ndoto zake.

Umeipata hiyo. Chukua hatua sasa upate nakala yako kwa kuwasiliana na 0655848392 sasa
Nakala moja ni 25,000/- tu.

Ijumaa Kareem


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X