/
Rafiki yangu aliwahi kuniambia kwamba kuna wakati aliangalia tamthiliya. Kwenye tamthilya hii kuna jamaa aliachwa na mke wake. Mke alimwacha kwa sababu jamaa hakuwa na hela.
Badala ya kukimbilia kuingia kwenye mahusiano mengine ili amuoneshe ex wake kwamba hajamkomoa kwa kuachwa. Jamaa aliamua kuanza kupambana ili kujenga biashara na kuzisaka hela.
Akapambana kwelikweli kiasi kwamba ikafikia hatu aambapo ex wake alikuwa ni shabiki wake kwenye vitu alivyokuwaanafanya.
Na siyo tu ex wake bali ex wake na mme wake wote kwa pamoja walianza kumshabikia jamaa.
Hiki ni kiwango cha mafanikio ambayo unapaswa kukipigani hasa unapoachwa kwa sababu huna hela. Badala ya kukimbili kufanya yale ambayo siyo ya muhimu. amua kwamba unaenda kuwekeza nguvu zako zote kwenye kutafuta pesa.
Badalaya kutafuta mchumba mwingine ili utambe kwa ex wako kuwa amekuacha kwa bahati mbaya, amua kwamba unaenda kuwekeza muda wako na nguvu zako kwenye kipaji, kujenga ujuzi au kitu ambacho kitakufanya kuwa mtu wa pekee.
Amua kuachana na kitu kingine chochote ambacho kitakuwa kinyume na hapo.
Ni kwa namna hiyo utaweza kujiondoa kwenye hali ya kuwa unaachwa kila wakati kwa ajili ya pesa rafiki yangu. Pambania malengo na ndoto zako kubwa kuanzia sasa.
Nakutakia kila la kheri.