Kitu Hiki Unapaswa Kukibadili Mara Moja


Moja ya siku ambayo watu huwa wanaadhimisha ni siku ya kuzaliwa. Ukiachana na sikukuu ya kuzaliwa kuna sikukuu maarufu sana ambazo huwa tunaadhimisha, ikiwa ni pamoja na Eid, Pasaka, Krismasi, Mwaka mpya na nyingine..

Ukiziangalia hizi sikukuu zote zina kitu kimoja ambacho kinaziunganisha. Hizi sikukuu zote huwa zinatokea kwa sababu ya kalenda. Ni sikukuu za kikalenda.

Hii nbdiyo kusema kwamba furaha yote ambayo huwa unakuwa nayo siku ya sikukuu hizi inatokana na kalenda. wewe hakuna juhudi zozote ambazo unaweka kuhakikisha sikukuu hizi zinatokea.

Utake usitake lazima tu sikukuu hizi zitakuwepo.

Hivyo, kufurahia kwenye sikukuu hizi ni jambo zuri lakini usisahau kuwa kitu unachoshangilia kwamba kimetokea hujakisababisha wewe. 

Ninachotaka uanze kufanyia kazi baada ya hapa ni wewe kuhakikisha unaanza kupambania malengo yako makubwa. Mwaka huu usiishie tu kushereheakea sikukuu ya kuzaliwa na sikukuu nyingine ambazo ziko nje ya uwezo wako. Yaani, sikukuu ambazo hujazisababisha wewe kutokea., Bali sambamba na mafanikio mengine ambayo utasherehekee mwaka huu basi uweze kusherehekea na mafaniko ambayo umeweza kusababisha mwenyewe.

Kuna kitu kimoja ambacho kama utakipambania unaweza kukileta kwenye uhalisia. Ni kitu gani hicho kimoja? hiki ndicho kitu pekee ambacho unapaswa kukipambania usiku na mchana na bila kukwama wala kuyumbishwa na mtu yeyote.

Kama utaanza kupambania malengo na ndoto zako leo, nakuhakikishia kuwa wanaoonak kama huwezi kufanyia kazi malengo na ndoto zako kubwa, kuna siku hawahawa watakuwa wanakushangilia kuwa umeweza kuzifanyia kazi ndoto zako mpaka zikaja kwenye uhalisia.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X