Leo ni jumatatu nzuri sana. Na kwa kuwa ni mwanzo wa wiki, una nafasi nzuri ya kuitumia siku ya leo kuchagua kitu kimoja ambacho utakifanya kwa msimamo wiki hii bila kuacha.
Kama wewe ni mwandishi, wiki hii unaweza kujiwekea utaratibu wa kuandika kwa wiki nzima bila ya kuwa na sababu yoyote ambayo inakuzuia wewe usiandike. Au unaweza kuamua kwamba lazima wiki hii kila siku, niandike sura moja ya kitabu na ikamilike. Wakati mwingine hatua kama hizi zinahitaji kujisukuma kidogo au kwenye nje ya mazoea uliyonayo, lakini ukweli ni kwamba hizi ni hatua ambazo uanapaswa kuzichukua hasa pale unjapokuwa umedhamiria kusongambele na kuhakikisha unafanya makubwa bila ya kukwama au kuyumbishwa na kitu chochote.
Ukweli ni kuwa kama unataka kufanya makubwa kuna wakati ambapo unapaswa kuchukua hatua kama hizi ili uweze kufikia mafanikio makubwa ambayo unataka.
Kama kwa mfano unataka kutoa kitabu siku za hivi karibuni basi unatakuwa kuahakiksiha kwamba unachukua hatu kama hizi ili uweze kutoa kitabu chako.
Ni kitu gani kimoja ambacho unaenda kukiwekea mkazo wan nguvu wiki hii?