rafiki yangu mpendwa salaam
leo nataka tuongelee ni njia ambazo unazitumia kuhakikisha kwamba unasambaza bidhaa zako? Una njia moja, mbili au zaidi!
Ninachotaka kukwambia siku ya leo ni kwamba kadri unavyokuwa na njia nyingi zaidi za kusambaza bidhaa zako ndivyo ambavyo unakuwa na uwezo wa kuwafikia wateja wengi kuliko pale unapokuwa na njia chache.
Hivyo kama unaweza kuwa na njia nyingi za kuwafikia wateja wengi, basi zitumie.