Upo tayari kuambiwa ukweli?


Rafiki yangu wa ukweli. Kama unaishi kwenye hii dunia, moja ya kitu ambacho huwezi kukikwepa ni watu kukusema. watu wanaweza kukusema kwa mazuri au kwa mabaya.

Moja ya kitu ambacho kamwe haupaswi kuogopa ni kusemwa. Kwenye hii dunia, kila mtu anasemwa, marehemu tu anasemwa, sasa wewe uliye hai unadhani itakuwaje?

Kama hakuna mtu yeyote anayekusema, hata nashindwa niseme nini juu yako, lakini naweza kusema HAUISHI. Unapaswa kuanza KUISHI.

SOMA ZAIDI: Kufa Leo, uishi milele

Na kwenye kusema wapo watakaokusema kwa uzuri, na wapo watakaokusema kwa ubaya. Wapo watakaokusema wakilenga uboreshe unachofanya ili kiweze kuwa bora zaidi, na wapo watakaokusema wakikukosoa kwa kukandamiza kila juhudi unazofanya.

Na kadiri unavyokuwa kiongozi au mtu wa ngazi za juu, ndivyo ambavyo kusemwa kwako kunakuwa kukubwa sana. Hivyo kwenye hilo eneo, usiogope kusemwa.

njia bora ninayotaka uangalie kusemwa huku ni kuangalia ukweli. Kama wanachosema watu kina ukweli wowote ndani yake, basi huo ukweli uchukue unakufaa. Kama wanaokusema wanalenga kukusaidia uboreshe unachofanya, usiwapuuze.

Ukweli mara zote huwa unabaki kuwa ukweli bila kujali nani anasema huo ukweli. Bila kujali ukweli huo umetoka kwenye kinywa cha nani. UKWELI NI UKWELI.

Kama wanaokusema wanalenga kukukosoa, ila wanachosema hakina ukweli wowote ndani yake. Yaani, labda wanasema hivyo ili wakuangushe hapo wapuuze na endeelea mbele kuweka juhudi kwenye kazi unazofanya.

rafiki yangu, mimi rafiki yako nakupenda sana na ninakutakia wakati mwema.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X