Je, kuna mtu amewahi  kukwambia kuwa hapa umekosea?


Je, kuna mtu amewahi  kukwambia kuwa hapa umekosea? Hili ni swali ambalo amewahi kuulizwa aliyekuwa rais wa marekani Donald Trump. Alijibu swali hili kwa kusema, kiuhalisia mke wangu huwa ananiambia kuwa nimekosea kila siku.

UKWELI NI KUWA kama kuna kitu cha tofauti ambacho unafanya kwenye maisha yako, ni lazima tu utaambiwa, tena utaambiwa  mara nyingi kuwa unakosea. Hasa pale unapokwenda kinyume na matarajio ya wengi. Pale unapokwenda kinyume na mazoea ambayo wengi wanakuwa wamejijengea kwenye maisha yao. Rafiki yangu wa ukweli, jiondoe kwenye haya mazoea ambayo wengi wamejiwekea kwenye maisha yao.

Anza kufanya vitu vya tofauti. Chukua hatua za tofauti hata kama wengine wanaona umekosea.

Wingi wa watu kusema kwamba umekosea haulalishi kukosea kwako.

Ila utakosea pale utakapoacha kufuata ndoto zako kubwa na malengo yako makubwa ambayo umejiwekea kwenye maisha.

Hakikisha unapata nakala ya kitabu cha JINSI YA KUFIKIA NDOTO ZAKO. Kupata nakala ya kitabu hiki ni rahisi sana.

Wasiliana nami kwa namba ya simu 0684408755 sasa ili ujipatie nakala yak oleo.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X