Rafiki yangu salaam, hongera sana kwa kazi. Mtu mmoja ameniuliza ni lini ninapaswa kukatia tamaa MALENGO na ndoto zangu.
Ni vigumu kidogo kujibu swali hili, lakini ukweli ni kuwa muda sahihi wa kukatia tamaa MALENGO na ndoto zako ni pale unapokuwa umetumia kila namna na kwa kila mbinu na Bado ukaona unakwama.
Ukweli ni kuwa unapoanzia kuyafanyia kazi malengo Yako Kuna vitu vingi ambavyo vitajitokeza mbele Yako.
Unapaswa kuwa tayari kukabiliana navyo. Siyo unakutana na ka changamoto kadogo tu, unakata tamaa.
Unapaswa kuwa tayari kupambana na kila kikwazo ambacho kinakuja mbele Yako bila ya kurudi nyuma.
Na kama kweli umemtumia kila njia na bado unaona mambo hayaendi ndiyo unaweza Kuliweka Hilo jambo pembeni na kuamua kupambania mengine.
Lakini jipe muda kwanza kwenye kulifanyia kazi lengo na ndoto zako bila ya kurudi nyuma.
Walau muda wa Miaka mifano mpaka kumi. Kama kweli ukiamuabkufanya jambo Moja kwa muda wa Miaka mifano mpaka kumi bila ya kukwama Wala kurudi nyuma. Nakuhakikishia kuwa hili jambo unaweza kulifanya kwa ukubwa zaidi ya unavyofikiri.
imeandikwa na Godius Rweyongeza
pata nakala ya kitabu Cha NGUVU YA VITU VIDOGO KUELEKEA MAFANIKIO MAKUBWA pamoja na kitabu Cha NGUVU YA KUWEKA MALENGO.
Kupata nakala wasiliana na mwandishi Sasa kwa 0755848391
asante