Unakuta mtu hajui ni kitu Gani anapaswa kufanya hapa duniani.
Lakini Bado anang’ang’ania kuwa anataka kwenda mbinguni. Huko mbinguni unataka kwenda kufanya Nini kama ya duniani yamekushinda.
Imeandikwa kuwa usipokuwa mwaminifu kwenye mambo madogo hutakuwa mwaminifu kwenye MAKUBWA. Kama usipokuwa mwaminifu kwa muda mchache wa hapa duniani. Unamwaminishaje Mungu kuwa mbinguni utautumia vyema ?
Kama tu maisha ya miaka michache ya hapa duniani yamekushinda, Sasa hayo maisha ya Kuishi MILELE utayaweza wewe? Huendi kuwa chokoraa huko mbinguni🤔
Ama kweli ukistaabu ya Musa, utayaona ya Filauni.