Jinsi Kufanya Majukumu Mengi Kwa Wakati Mmoja Kunavyokupotezea muda badala ya kusevu muda


Rafiki yangu unaendeleaje, 

Kuna wakati unajikuta una majukum mengi na hivyo kuona ufanye majukumu hata mawili kwa wakati Mmoja ukidhani kuwa utarahisisha kufanikisha majukumu Yako kwa wakati.

Hata hivyo nataka nikwambie kuwa kufanya Majukumu Mengi Kwa Wakati Mmoja kunakupotezea muda mwingi. Kazi ambayo ungeifanya kwa muda mfupi unajikuta unaifanya kwa muda mrefu.

Ngoja nikupe mfano mzuri.

Ebu Sasa hivi andika sentensi

Kufanya Majukumu mawili kwa wakati mmoja ni kupoteza muda

Umetumia sekunde ngapi  Kuandika hiyo sentensi?

Chini yake andika sentensi nyingine pia. Andika hivi; 

Sasa nimeelewa

Umetumia sekunde ngapi Kuiandika na hiyo?

Sasa nataka hizi sentensi mbili uziandike kwa wakati mmoja.

Yaani uandike, 

Kufanya Majukumu mawili kwa wakati mmoja ni kupoteza muda

Na 

Sasa nimeelewa kwa wakati mmoja

Andika herufi Moja Moja ya kila sentensi kwa kubadilishana.

Anza sentensi ya kwanza kwa Kuandika

K

Na kwenye sentensi ya pili andika

S

Endelea kuandika herufi Moja Moja kwa kila sentensi kwa kubadilishana mpaka kila sentensi ikamilike. Utagundua kwamba umetumia muda mwingi kwenye kuandika pale unapokuwa unaandika sentensi mbili kwa wakati mmoja. Unaweza kutumia muda mpaka mara kumi zaidi ya muda wa kawaida

Kumbe ujumbe tunaoondoka nao Leo ni kwamba tusifanye majukum mengi kwa Wakati Mmoja, badala yake tujikite kwenye jukumu Moja kwa wakati, tulikamilishe kabla ya kwenda kwenye jukumu jingine.

 Imeandikwa na 

Godius Rweyongeza 

0755848391

Morogoro Tanzania


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X