Kitu Ambacho Kinaua Biashara Nyingi


Kuna utafiti ambao ulifanyika, na ulikuja na majibu ya kitofauti kidogo ambayo huwezi kuyategemea.  Utafiti huu ulihusisha wateja, wafanyakazi pamoja na viongozi wa kampuni na biashara mbalimbali.

Lengo la utafiti huu lilkuwa ni kuona ni kwa namna gani kampuni au taasisi zinatoa huduma bora kwa wateja. Asilimia kubwa ya viongozi wa kampuni zilizofanyiwa utafiti walisema kwamba wanatoa huduma bora kwa asilimia 95%. Walijiona kwamba wako vizuri kwenye kutoa huduma kwa wateja.

Aidha walipoulizwa wafanyakazi waeleze kiwango chao cha kutoa huduma kwa wateja,  walisema kwamba, wanatoa huduma bora kwa asilimia 75.

Kitu cha kushangaza kilikuja pale walipoulizwa wateja wanaonunua kwenye kampuni au taasisi husika. Hawa walisema kwamba huduma wanayopata kwenye kampuni au taasisi husika ni ya viwango vya asilimia 8% tu.

Kumbe wakati viongozi kwenye kampuni husika walikuwa wanajiona vizuri, wakati wafanyakazi walikuwa wanajiona vizuri, wateja walikuwa bado wanaona kwamba kuna mambo mengi ambayo hayajakaa sawa ambayo watu hao wanapaswa kurekebisha. Kitu hiki inawezekana kinatokea kwako pia. unaweza kuw aunajiona vizuri kwenye huduma kwa wateja au kwenye biashara yako, lakini badala ya kujiona kwamba uko vizuri sana. Jichukulie kwamba kuna mambo mengi ambayo hujafanya na unapaswa kuyafanya.

Jione unatoa huduma kwa asilimia 8 tu

Rafiki yangu, badala ya kujiona kwamba unatoa huduma bora kwa asilimia 95 au 75, jione unatoa huduma kwa asilimia 8, kisha kazi yako iwe ni kuangalia ni kwa namna gani unaweza kutoka kwenye hiyo asilimia 8 na kwenda mpaka asilimia 95 na zaidi. Usijione umefika, jione bado unapaswa kuendelea kupambana kushinda muda wote.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X