
Dr. Myles Munroe ni mmoja watu ambao walikuwa wamefanikiwa sana kwenye sekta ya maendeleo binafsi. Kazi zake nyingi zimegusa maisha ya watu wengi enzi za uhai wake mpaka leo hii. Siku moja alikuwa anaeleza namna alivyoenda kwenye duka la vitabu na kununua kitabu cha zaidiya dola 125. Dola 125 ni zaidi ya laki mblii na nusu za Tanzania.
Msaidizi wake alishangaa kuona kwamba Dr. Myles Munroe amenunua kitabu cha gharama kubwa hivyo. Kwa nini unatumia gharama kubwa hivyo kununua kitabu kimoja tu? Kw anini usitumie hii hela kufanya vitu vingine kama kununua nguo? Hapo ndipo Dr. Myles Munroe alipomwambia msaidizi wake kwamba, hiii ndiyo tofauti inayotutofautisha mimi na wewe. Ndiyo maana mimi ni kiongozi na wewe ni mfuasi. Unajua kwa nini alimwambia hivyo? Alimwambia hivyo kwa sababu alijua wazi mazuri yaliyo kwenye vitabu ambavyo msaidiz wake alikuwa bado hayajui.
Ukweli ni kuwa kwenye maisha ya kila siku ni kwamba unapaswa kuwa mtu ambaye anajifunza bila ukomo. Wekeza nguvu na muda wako kwenye kujifunza mara kwa mara bila ya kuchoka. Kamwe usifikie hatua ambapo utajiona kwamba umejifunza na umeju akila kitu kwenye maisha yako. kila mara unapaswa kuwa unaendelea kujifunza bila ya kukoma. Kujifunza ni tiketi ya wewe kufanya makubwa. Kujifunza kunakufanya unaona mbali kuliko pale ambapo unakuwa hujifunzi.
Kwenye haya maisha, kubali watu wakuite mzembe, ila siyo kwenye vitu viwili. Kwanza usikubali kuitwa mzembe kwenye kufanya kazi kwa bidii, na usikubali kuitwa mzembe kwenye kujifunza. Hivi ni vitu viwlii ambavyo unapasw akuwa unavipambania kila siku, bila ya kuacha na bila ya kujali kitu gani ambacho kinatokea kwenye maisha yako. hakikisha mara zote unapambana kushinda kila siku kwenye haya maeneo mawili.
Makala hii imeandikwa na Godius Rweyongeza
unaweza kujifunza zaidi kutoka kwa Godius Rweyongeza kwa Kujiunga naye hapa