Msimamo na mwendelezo


Rafiki yangu moja ya kitu cha muhimu sana kwa wewe unayetaka kufanya makubwa ni kuwa na mwendelezo kwenye kitu ambacho unafanya. Wengi huwa wanaweza kufanya kitu mara moja, ila siyo kwa mwendelezo. Wewe unahitaji kuwa na mwendelezo kwenye kazi na shughuli zako zote unazofanya.

Ukianzisha kitu, usikifanye mara moja tu. Bali kifanye kwa mwendelezo kwa siku nyingi zinazofuata. Mafanikio ya kweli yapo kwenye kufanya vitu kwa mwendelezo ba siyo kufanya mara moja tu.

Wengi huwa wanaweza kuanza kuweka akiba, ila siyo wote wanaweza kuwa na mwendelzo kwenye kuweka akiba.

Wengi huwa wanaweza kuanza kufanya mazoezi, ila siyo wote ambao huwa wanakuwa na mwendelezo kwenye kufanya mazoezi. Wengi huwa wanaweza kuanza kunoa vipaji vyao, ila siyo wote ambao huwa wanakuw ana mwendelezo kwenye hilo.

Na kwa sababu tu ya kukosa mwendelezo wengi huwa wanaishia kujishangaa kwa nini hawapati matokeo na mafanikio makubwa. Kumbe kinachowafanya wasipate mafanikio makubwa ni kwa sababu hawana mwendelezo kwenye kufanya kile ambacho wanaamua kufanya.

Sasa rafiki yangu naomba nikwambie kitu kimoja muhimu sana. Kwa kitu chochote ambacho utachangua kufanya mwaka huu, hakikisha kwamba unakuwa na mwendelezo. Usifanye kitu na kuishia njiani. Bali kifanye kwa msimamo na kwa muda mrefu.

Tukimwangalia mtu kama Warren Buffet ambaye amekuwa anawekeza tangu ana miaka 11 mpaka leo hii, tunachojifunza kwake ni kwamba amekuwa anawekeza kwa mwendelezo na kwa msimamo.

Tukisoma historia ya mtu kama Kobe Brayant tunagundua kwamba alikuwa anaamka mapema na kuanza kufanya mazoezi, na anachelewa kulala. Na hii ndiyo ilikuwa ratiba ya kila siku. Unachogundua hapo ni mwendelezo.

Au hata ukisikia Michael Jordan anasema kwamba, nimeshindwa mara nyingi sana ndiyo maana nashinda. Ni kwa sababu anakuwa na mwendelezo.

Wewe pia kuwa na mwendelezo kwenye kitu ambacho unafanya.

Usifanye kitu mara moja tu.

Usifanye mara mbili. Hapana

Fanya kwa mwendelezo na kwa msimamo. Kwa muda mrefu bila kuacha.

Makala hii imeandikwa name rafiki yako wa ukweli.

Godius Rweyongeza

Tuwasiliane sasa kwa namba ya simu 0755848391

Karibu sana


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X