Rafiki yangu, kwenye makala ya jana nilikusisitiza kitu kimoja muhimu sana. Kitu hiki ni kufanya kila unachofanya kwa msimamo, na kwa mwendelezo. Kama hukusoma hii makala, rudi hapa uisome kwa umakini mkubwa.
Msimamo na mwendelezo.
Kitu hiki ni kutokuacha kufanya kitu husika zaidi ya mara mbili. Ikitokea kuna siku umeshindwa kufanikisha kitu fulani ambacho umepanga kufanya, basi walau kesho yake usishindwe kufanya hivyo.
Usikose mara mbili. Kosa leo ila siyo na kesho pia.
Pambana kadiri ya uwezo wako kuhakikisha haukosi kufanya jambo ulilopanga kufanya mara mbili mfululizo.
Kama umepanga kuweka akiba, pambana uwezavyo usiache kuweka akiba mara mbili mfululizo. Kama umepanga kuwekeza, pambana kadiri iwezekavyo ushindwe kufanya hivyo mara mbili mfululizo.
Ukiona umekosa siku ya kwanza, kufanya jambo fulani. Ukaona na siku ya pili pia hujaweza kufanya hivyo, basi ujue wazi kuwa hutaweza kuwa na mwendelezo kwenye jaambo lako na itakuwa vigumu kwako kuweza kufikia mafanikio makubwa
Sasa swali la pekee ambalo n ingependa kukuacha nalo siku ya leo ni kwamba, ni kitu gani ambacho umekuwa unatamani kufanya kwa mwendelezo? Na ni kwa namna gani unaenda kukifanyia kazi kuanzia sasa hivi?
Tukutane kwenye makala ya kesho