Sizungumzii mwezi wa Ramadhan, wala Kwarezima. Nazungumzia mfungo.
Kwamba kuna kitu ulikuwa unafanya, ila kinakutoka kwenye mstari wa kufanyia kazi malengo na ndoto zako kubwa. Sasa unaamua kwamba nafuga na ninaacha kukifanya kwa wiki moja.
Kwa mfano ulikuw aunatumia muda mwingi facebook, au youtube au tiktok, unaamua sasa kwa wiki moja ijayo naondoa hii tiktok kwenye simu yangu, na muda ambao nilikuwa nautumia huku ngoja niuweke kwenye kazi.
Yaani, kwamba ile tabia ambayo huipendi, ambayo inakukwamisha unaachana nayo, unajenga tabia mpya, nzuri ya kukufanya usongembele.
Hii unaweza kuifanya hata leo….Usisubiri mwezi wa ramdhan au Kwarezima.
Hivi ndivyo utazidi kuwa bora kwenye maisha yako, hivyo ndivyo utazidi kufanya mazuri na kuwa imara zaidi.
Ni kitu gani ambacho unaenda kufunga kuanzia siku ya leo?
Tujadiliane hapa chini