Kwenye mojawapo ya kitabu cha Robert Kiyosaki, ameandika kwamba watu wengi huwa wanapambana kuweka malengo ila huwa wanasahau kitu kimoja muhimu sana. na kitu hiki siyo kingine bali ni mchakato wa kufanyia kazi malengo na ndoto ambazo mtu unakuwa nazo.
Kumbe moja ya changamoto ambayo inawakumba watu wengi wanaoweka malengo siyo tu kuweka malengo, bali ni kuweka malengo na kutoyafanyia kazi. suluhishio la hili ni kuwa n mchakato kamili wa kufanyia kazi malengo yako mpaka yatimie. Na hapa ndipo unakuja huo usemi unaosema kwamba mchakato ni bora zaidi kuliko malengo.
Unajua kwa nini watu wengi huwa wanaweka malengo kwa mfano malengo ya kuweka akiba ila bado huwa wanashindawa kuyafanikisha ilihali malengo hayo huwa ni mazuri na ya kupendeza. Ukweli ni kwamba mchakato wa kufanyia kazi malengo hayo ndiyo huwa unakosa.
Kumbe, mchakato wa kufanyia kazi malengo na ndoto zako ni bora zaidi kuliko malengo yenyewe.
Unapokuwa na mchakato maana yake, malengo yako unayapa nguvu. malengo yako unawekea mfumo wa kufanyika hata kama haupo. malengo yako unayapa uhai.
Mfano kama lengo lako ni kuweka akiba. unaweka mfumo wa kukata hela kwenye akaunti yako kila inapoingia. au kila baada ya muda fulani. hapo unakuwa umeweka mchakato. na mchakato huu utakuwezesha wewe kufanikisha lengo lako bila wasiwasi wowote. Ndiyo maana nakwambia kwamba mchakato ni bora zaidi kuliko hata lengo lenyewe unalokuwa nalo.
SASA SWALI la kujiuliza siku ya leo ni kwamba je, una malengo yoyote ambayo umeyaweka kwenye maisha yako. kama una malengo, basi ni jukumu lako kuhakikisha kwamba unayawekea mchakao wa kuyafanyia kazi haya malengo bila kuacha.
kama utakwama kwenye kuweka mchakato wa kufanyia kazi malengpo yako, basi tunaweza kuwasiliana sasa. Tuwasiliane kupitia barua pepe godiusrweyongeza@gmail.com ili niweze kukusaidia kwenye hilo.
Kumbuka kwamba lengo lolote lile unaloweka, linaweza kuwekekewa mchakato wa kulifanyia kazi. changamoto inakuwa tu pale unapokuwa hujui namna ya kuweka mchakato kwenye lengo lako ili liweze kufanikiwa. lakini fahamu wazi kuwa mchakato wa kufanyia kazi malengo na ndoto zako kubwa, ni bora zaidi kuliko malengo yenyewe.
KUMBUKA Pia kwamba, kama hujui namna ya kuweka mchakato halisi wa kuweka malengo, basi unaweza kuwasiliana nami ili niweze kukusaidia kwenye hili.
Ni mimi rafiki yako
Godius Rweyongeza
07555 848 391
Morogoro-Tz