Katika safari ya maisha, watu wengi hutamani kubadilika, kuboresha maisha yao, na kufikia mafanikio makubwa. Lakini wengi hukata tamaa baada ya miaka kupita bila kuona tofauti kubwa. Swali ni: kwa nini baadhi hubadilika na kupiga hatua, huku wengine wakibaki vilevile?
Msemaji na mwandishi maarufu, Charlie “Tremendous” Jones, alitoa kauli yenye nguvu sana:
“Miaka mitano kuanzia sasa, utakuwa mtu yule yule wa leo isipokuwa kwa watu uliokutana nao na vitabu ulivyosoma.”
Hii si tu kauli nzuri ya motisha ni kanuni ya maisha. Inatufundisha kuwa mabadiliko ya kweli hayatokei kwa bahati, bali kwa maamuzi ya kila siku ya kujifunza na kujizunguka na watu sahihi.
1. Watu Uliokutana Nao: Msingi wa Ukuaji wa Kijamii na Kiakili
Watu tunaowaruhusu kuingia kwenye maisha yetu wanaweza kutuinua au kutuvuta chini. Marafiki, washauri, wakosoaji, na hata wapinzani wote huathiri namna tunavyofikiri, tunavyoongea, na tunavyotenda.
- Kukutana na mtu mwenye maarifa kunaweza kufungua milango ya fursa mpya.
- Mshauri mzuri anaweza kukuokoa na makosa ambayo yangegharimu miaka ya maisha yako.
- Rafiki mbaya anaweza kuchelewesha ndoto zako kwa kukushawishi kushughulika na mambo yasiyo na maana.
Jiulize: Ni watu wa aina gani nimewakaribisha katika maisha yangu? Wananisaidia kukua au wananikandamiza?
2. Vitabu Ulivyosoma: Mbegu za Mabadiliko ya Akili
Kitabu kizuri kinaweza kubadilisha fikra zako milele. Kinaweza kukuamsha toka usingizini wa kiakili na kukuonyesha namna mpya ya kuona dunia. Kusoma ni kama kuzungumza na watu wakuu ambao huenda huna nafasi ya kukutana nao ana kwa ana.
- Kitabu cha kifedha kinaweza kukuonyesha namna ya kutoka kwenye madeni.
- Kitabu cha motisha kinaweza kukuamsha uanze kuchukua hatua ulizokuwa unahofia.
- Kitabu cha maarifa kinaweza kukufanya kuwa mtaalamu katika eneo fulani na kukuongezea kipato.
Jiulize: Ni vitabu gani vimenisaidia hadi sasa? Na ni vitabu gani ninahitaji kuvipitia ili kufikia ndoto zangu?
3. Chukua Hatua: Fanya Uchaguzi wa Kukua
Usingoje miaka mitano ipite bila mabadiliko. Anza leo kwa:
- Kutafuta watu chanya wanaokutia moyo, wanaojua zaidi yako, na wanaotamani kuona unafanikiwa.
- Kujipangia mpango wa kusoma angalau kitabu kimoja kila mwezi. Hata ukianza na kurasa chache kwa siku, utaona matokeo.
Miaka mitano si mbali. Itafika, iwe umebadilika au la. Swali ni: utakuwaje baada ya miaka hiyo? Utakuwa mtu mpya, mwenye fikra kubwa, malengo makubwa, na hatua kubwa au utakuwa bado unalalamikia maisha yale yale?
Jibu liko mikononi mwako. Anza leo kukutana na watu sahihi na kusoma vitabu bora. Hapo ndipo mabadiliko ya kweli huanzia. Na kama unataka kupata vitabu vya kweli vya kubadili maisha yako. Tuwasiliane sasa kupitia 0755 848 391 au 0684408755
Pia nichukue nafasi hii kukukaribisha kwenye channel yetu ya telegram ambapo naweka makala mpya kila siku ambazo unaweza kuzitumia kujifunza na kuchukua hatua. Jiunge na channel yetu hapa.
Je, upo tayari kuwekeza katika mabadiliko yako?
Tuandikie vitabu gani vimekugusa au ni watu gani wamekuwa chachu ya mafanikio yako. Tunapenda kusikia kutoka kwako! Tuandikie kwenye email ya songambele.smb@gmail.com
Pia usisahau kujiunga na semina yetu ya mwezi huu wa sita ambayo itafundisha mambo mengi kwa undani.
One response to “Siri ya Mabadiliko ya Kweli. Miaka Mitano Ijayo Utakuwa Jinsi Ulivyo Isipokuwa Kwa Vitu Hivi Viwili”
[…] makala ya jana rafiki yangu. Niliandika Siri ya Mabadiliko ya Kweli. Miaka Mitano Ijayo Utakuwa Jinsi Ulivyo Isipokuwa Kwa Vitu Hivi Viwili. Baada ya kuelewa kuwa watu unaokutana nao na vitabu unavyosoma vina mchango mkubwa katika […]