Hongera sana kwa kuendelea kupambana rafiki yangu.
Kwenye MAISHA Kuna wakati mambo yanakuwa yanaenda ndivyo sivyo. Mipango Yako unaenda kinyume na matarajio Yako.
Leo ningependa nikwambie tu, inapotokea mipango Yako umependa kinyume, fahamu kuwa
1. Unapaswa kukaa chini na kujitafakari upya. Kushindwa au kuanguka si KITU kibaya, ubaya ni pale unapokataa kukaa chini na kujifuñza kutokana na kushindwa huko. Hivyo Kaa chini ujitafakari, umeshindwa wapi? Kwa Nini umeshindwa? Ni KITU Gani unaweza kufanya ili utoke hapo na kwenda HATUA ya ziada? Tumejifunza Nini?
2. Panga upya. Kila unapojitafakari, panga upya, uone ni HATUA Gani zaidi utachukua baada ya hapo? Ni nini unaenda kufanya baada ya hapa?
3. Chukua HATUA kimkakati zaidi? Baada ya kuwa umeanguka, tayari umeshajua wapi umekosea, kinachofuata ni wewe kuanza kufanyia kazi malengo Yako kimkakati zaidi?
4. Jifanyie tathimini Kila mara. Kila mara jifanyie tathmini kuona mwenendo wako. Uko wapi, unaelelea wapi na Nini zaidi tunafanya.
Imeandikwa na Godius Rweyongeza
0755848391