Kama huwezi kupaa, kimbia


RAFIKI yangu mpendwa salaam, nichukue nafasi hii kukupongeza kwa kazi nzuri unayofanya.

Moja ya kitu ambacho kimekuwa kinawakwamisha watu wengi kuandika ni kwa sababu hawana vifaa vya kuandikia. Ukweli ni kuwa muda mwingine si kwamba unahitaji kuwa na vifaa vya kipekee sana ili uandike, bali unapaswa uanze kuandika kwa kutumia vifaa ulivyonavyo.

ANZA KUANDIKA kwa kutumia simu yako. Asilimia kubwa ya watu wanamiliki simu. Wewe kama mwandishi, itumie simu yako kuandika. weka app za kutumia kuandika kwenye simu yako, kama app ya Google docs kisha anza kuandika.

HARIRI kitabu chako kwa kutumia simu yako. Baada ya kuandika, anza kuhariri kitabu chako kwa kutumia simu yako hiyohyo.

Tengeneza Kava kwa kutumia simu. App ya Canva inaweza kukusaidia kwenye kutengeneza kava na hata kwenye kupangilia kitabu chako.

SANIFU kitabu chako kwa kutumia simu yako pia. Inawezekana kutumia simu yako kwenye kusanifu maudhui na mwonekano wa ndani ya kitabu pia.

Lakini pia kama una vifaa zaidi ya simu unaweza kuvitumia rafiki yangu.

Ninachoweza kukwambia ni kwamba kwenye kuandika, tumia kile ulichonacho.

Kama huna simu, andika kwenye daftari.

kama huna tablet, tumia simu

kama huna kompyuta, tumia tablet.

ila kwa vyovyote vile usiache kuandika.

Ningependa tu kukuuliza swali moja, ni lini utaweza KUANDIKA KITABU CHAKO NA KUKIKAMILISHA?

SOMA ZAIDI: Vitu 50 Ambavyo Hupaswi Kuchukulia Poa


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X