
Mwaka 2025 kwa hapa kwetu Tanzania ni mwaka wa UCHAGUZI. Na tayari hivi ninavyoandika hapa kampeni zimeanza nchi nzima. Wagombea wote wanajinanadi uwachague waende kukuwakilisha kwa miaka mitano ijayo.
Mtu yeyote anayekuja kwako kuomba kuchaguliwa lazima tu atakuja sera. Atakuuzia wewe sera, ukiona zinafaa maana yake utanunua hizo sera kwa kumpigia kura.
Unapomchagua mtu yeyote, maana yake unampa mamlaka ya kwenda kutekeleza sera hizo kwa kipindi cha miaka mitano. UCHAGUZI Huwa ni KILA BAADA YA MIAKA MITANO.
Kwa nini miaka mitano?
Iko hivi, miaka mitano ni kipimo ambacho tunaenda kuona kama mtu alichoahidi amekifanyia kazi au la. Hii ndiyo kusema kwamba yeyote anayechaguliwa anapewa MUDA wa kutosha kufanilisha jambo lake kwa sababu MAFANIKIO ni mchakato. Si KITU Cha siku Moja au mbili.
MALENGO+MUDA=MAFANIKIO
Ndiyo maana malengo yanahitaji muda, na wanaochaguliwa wanapewa muda wa kutekeleza sera zao.
Tunahitaji tuchague Watu wazuri wa kutuongoza na hapa nataka nikwambie mtu mmoja ambaye unapaswa kumchagua kwa uhakika. Mtu huyu atakufaa sana.
Unajua ni nani huyu?
Nisikilize kwa haya kwanza.
Iko hivi, unapomchagua diwani, mbunge au rais maana yake unakuwa umempa kazi. Kwamba KILA siku ukiamka fikiria kuhusu haya unayoniambia, na kila siku ukienda kulala, fikiria kuhusu hayahaya.
Yaani, kazi yake ni hiyo. Anapaswa kuachana na mengine yote na kuweka NGUVU kubwa kwenye sera au ilani aliyotoa.
Sasa twende kwa mtu unayepaswa kumchagua. Mtu huyu si mwingine Bali ni wewe. Unapaswa kujichagua KWANZA. JICHAGUE MWENYEWE 2025
Kivipi? Pengine unajiuliza yaani Mimi najichaguaje? Mbona Sina sera wala ilani yoyote?
Na hapa ndipo narudia tena kwa kusema kwamba JICHAGUE MWENYEWE. Ni mambo yapi ambayo kila siku kwa miaka mitano ijayo, kila utakapokuwa unaenda kulala utakuwa ukiyafikiria, na ni mambo yapi kwa miaka mitano ijayo kila ukiamka utakuwa ukiyafikiria. Hizi ndizo sera zako
Kabla hujaenda kumpigia kura diwani yoyote. Kabla hujaenda kumpigia kura mbunge wala rais, JICHAGUE. Unajichagua vipi?
Kuwa na sera au ilani? Yaani MALENGO Yako unayoenda kuyafanyia kazi usiku na mchana kwa miaka mitano ijayo. Ikumbukwe tokea mwanzo ninesema kwamba unapomchagua kiongozi maana yake KWA miaka mitano ijayo KILA akiamka anakuwa anafanyia kazi sera au ilani zake Ili zitimie.
Sasa swali langu kwako siku ya Leo ni kwamba SERA ZAKO ZA MIAKA MITANO IJAYO NI ZIPI? MALENGO YAKO AMBAYO YATAKUAMSHA KILA SIKU UKIENDA KUYAPAMBANIA NI YAPI?
Kama huna haya, hii miaka mitano inaenda kupiga, utakuwa hujafanya chochote Cha maana, na kama kulalamika utakuwa unalalamika maisha magumu. Ukweli mchungu ni kwamba bila kujali ni kiongozi Gani ynaenda kumchagua, kama wewe mwenyewe huna MALENGO Yako ya kutoboa, huyu kiongozi hata kufanya utoboe. Ni mpaka pale utakapokuwa na malengo Yako.
Bahati wanakutana nayo walio kwenye mwendo na siyo wale waliotulia.
Unapoweka MALENGO maana yake umeamua kuwa kwenye mwendo.
Sasa hata kama huna MALENGO basi kwa miaka mitano ijayo, hakikisha unafanyia kazi haya MALENGO
MOJA, KUAMKA MAPEMA. Niwekee utaratibu wa kuamka walau saa 11 kwa miaka mitano ijayo na siyo zaidi ya saa 12 KASORO.
MBILI, KUSOMA VITABU, kwa miaka mitano ijayo soma walau kurasa kumi za kitabu KILA siku. Hii itakusaidia
TATU, KUWEKA AKIBA, kwa miaka mitano ijayo weka akiba walau ya sh elfu Moja tu KILA siku.
NNE, KUWEKEZA KWENYE HISA, HATIFUNGANI Au VIPANDE. Kwa miaka mitano ijayo, chagua KUWEKEZA pia. Anza na Uwekezaji kwenye HISA na siku hizi unaweza kununua hisa kiganjani mwako kupitia app ya DSE KIGANJANI.
TANO KUFANYA KAZI KWA BIDII, kwa miaka mitano ijayo, chagua kuwa kazi ndiyo kitu pekee ambacho kinaenda kukutambulisha. Kazi huwa haidanyanyi na kamwe usifeli kwenye hilo.
Nakuhakikishia BAADA ya miaka mitano utakuwa mmoja wa Watu watakaokuwa wanamiliki uchumi wao wa maana.
Rafiki yangu, tunayo miaka mitano ya uhakika mbele yetu. Ni au uchague kuitumia vizuri au la unaenda kuipoteza. Chagua kuitumia vizuri Sasa.
Imeandikwa nami rafiki yako wa ukweli
Godius Rweyongeza
Karibu sana.
Makala hii imeandikwa na Godius Rweyongeza
Jipatie vitabu vya Godius Rweyongeza kwa kuchagua HAPA.
Hakikisha umepata kitabu cha RASILIMALI ZA WATU WENGINE, ni kitabu kizuri kwa ajili yako. wasiliana na 0755848391 au 0745848395 sasa
Makala ya kesho itawekwa kwenye blogu ya SONGAMBELE ambayo unaweza kuifikia kupitia www.songambele.co.tz na itawekwa kwenye channel ya telegram pia ambayo unaweza kuifikia kwa KUBONYEZA HAPA