Biashara ni Mkakati, Wa Kwako Ni Upi?


Biashara huwa zinakuwa na mkakati wa biashara. Inawezekana wewe mwenyewe hujui kwamba una mkakati kwenye biashara, lakini kutoujua mkakati huo, haimaanishi kwamba haupo. Upo tu, tena umejaa tele. 

Mkakati wa biashara tunaweza kuuona kwenye namna unavyofanya shughuli zako kwenye biashara yako. Sasa swali ni je, mkakati wa biashara unapaswa kugusa kitu gani na kitu gani?

Washiriki wa semina ya Godius Rweyongeza
Washiriki wa semina ya Godius Rweyongeza

Kwenye biashara, mkakati wa biashara unaweza kuwa

  1.  KIla mmoja kwenye biashara kujua anachopaswa kufanya na lini kinapaswa kuwa kimekamilika na kukifanya kwa bidii, 
  2. Kila mmoja anapaswa kuwa anashambulia muda wote. Hakuna timu ya mpira wa miguu ambayo huwa inashinda kwa kulinda lango bali kwa kushambulia.
  3. Kuwa bora kwenye eneo fulani, bidhaa moja au huduma moja ambayo utafahamika kwayo kabla hujaanza kuzalisha bidhaa nyingine au huduma nyingine.
  4. Ni muhimu sana kwenye biashara kuhakikisha kwamba unatafuta njia ambayo ni bora, haraka, urahisi na ya uhakika kwa wateja.
  5. kwenye biashara kampuni zina watu wanaojituma kwenye kazi. Wanatumia neno kama sisi. Wanaona kampuni kama mwendelezo wao. na hawafikirii kwamba hiyo siyo kazi yangu.
  6. Kwenye biashara kila mara unaangalia namna ya kumshangaza mteja kwa kumpa huduma bora, ya haraka ya uhakika na 
  7. Kwenye biashara unatakiwa kulijua soko lako na kutengeneza mbinu za uhakika za kulifikia hili soko lako bila shida yoyote.

hii ni baadhi ya mikakati muhimu sana unayoweza kuwa nayo.

Ni mkakati upi unaenda kuanza nao siku ya leo?

Makala hii imeandikwa na Godius Rweyongeza

Jipatie vitabu vya Godius Rweyongeza kwa kuchagua HAPA.

Wasiliana nami wasap hapa

Hakikisha umepata kitabu cha RASILIMALI ZA WATU WENGINE, ni kitabu kizuri kwa ajili yako. wasiliana na 0755848391 au 0745848395 sasa

Makala ya kesho itawekwa kwenye blogu ya SONGAMBELE ambayo unaweza kuifikia kupitia www.songambele.co.tz na itawekwa kwenye channel ya telegram pia ambayo unaweza kuifikia kwa KUBONYEZA HAPA


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X