Unapokosea Wewe Ni Hapa


Kwenye makala ya Jana nilisema kwamba kabla hujamchagua kiongozi yeyote mwaka huu, JICHAGUE MWENYEWE kwanza. Una dira ya miaka mitano ijayo, kama huna iweke Kisha JICHAGUE na kila siku ukiamka kwa miaka mitano itekeleze.

Sasa Moja ya KITU ambacho Watu wanajiambia ni kuwa nikifa je? Ni bora nisiweke mipango ya miaka mitano maana naweza kufa.

Ukweli ni kuwa

Ukweli wa kwanza: wanaoweka mipango siyo kwamba hawafi na hatuweki mipango kwa sababu hatuji kufa.

Ukweli wa pili: kutokuweka mipango kunakuweka kwenye nafasi ya kufa haraka kweli. Unaweza kudhani kujiambia ajuaye kesho ni Mungu ni njia nzuri ya kuishi, ila ukweli ni kuwa unajiua. Iko hivi, unapokuwa na mipango maana yake unaenda kuwa bize muda wote. Unaepuka vishawishi, unaepuka vitu ambavyo vinaweza kukuingiza matatani, ila unapokuwa huna malengo, kila kitu kinakuwa lengo kwako. Kuna wakati unaweza kujikuta unajadili mambo ya watu, si unajua akili tupu ni karakarana ya shetani.

Iko hivi, kama huna mipango, maana yake huna Kusudi la kufanyia kazi na watu ambao hawana Kusudi hufa mapema. Hivyo, kutokupanga ni kupanga kujiua.

Ukweli wa tatu: unambebesha Mungu mzigo ambao sio wake.
Kuna watu kila kitu wanasema Mungu anajua, yaani mpaka wanamfanya Mungu anajuta kuwaumba. Hawawezi kufanya maamuzi yoyote, hawawezi kuchukua hatua pale wanapotakiwa kufanya maamuzi, wanachofanya ni kwamba wanasubiri tu Mungu afanye.

Ninachotaka wewe ufahamu ni kuwa ni kweli Mungu anafanya pale na wewe unapofanya. Usimbebeshe Mungu mzigo ambao unapaswa kuufanya wewe. kazi ya kuweka malengo na mipango ni ya kwako. Hiyo usimbebeshe Mungu, ibebe wewe mwenyewe. Kazi ya kuibadili kesho yako na kutengeneza kesho bora ni ya kwako. Ni jukumu lako kuhakikisha kwamba unalipambania hili suala.
Kesho inayong’aa inatengenezwa sasa hivi.

SOMA ZAIDI: AMSHA UUNGU ULIO NDANI YAKO: Sifa 3 Za Kimungu Unazopaswa Kuzitumia Kuanzia Leo

Imeandikwa nami rafiki yako
Godius Rweyongeza
0755848391
Morogoro-Tz

 


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X