Ijue Siri Ya Babiloni Kuwa Mji Tajiri Kuliko Yote Duniani


Babiloni ulikuwa mji katika sehemu ya Mesopotamia. Mji huu ulikuwa sehemu ambayo ni kame na hivyo haukuwa na mvua za kutosha ili kuweza kuendesha shughuli yoyote ya kilimo.
Chanzo pekee cha maji kilikuwa ni mto Euphrates.
Watu wa Babiloni waliweza kuchimba mifereji kuingia mjini mwao na hivyo kuendesha shughuli zao za kuwaingizia kipato.

Jambo kubwa lililowafanya kuwa matajiri ni kwa sababu walikuwa wanatunza moja (1/10)  ya kumi ya kile walichokuwa wanaingiza.Kwa lugha nyingine unaweza kusema walikuwa wanajilipa kwanza.

Kujilipa kwanza ni kutoa moja ya kumi ya kile unachoingiza kama kipato na kuweka kama akiba.

Kuweka moja ya kumi ya kile unachoingiza kama kipato,itakufanya baada ya mda fulani kuwa umeweka pesa ya kutosha kuweza kuanzisha biashara ambayo unaifikiria au kuweza kuwekeza sehemu flani.
Ukipata shilingi 1000 usitumie yote weka shilingi 100 ambayo ndo moja ya kumi yake kama akiba.
Ukipata shilingi 10,000 usitumie yote weka shilingi 1,000 ambayo ndo moja ya kumi  kama akiba.
Ukipata laki moja weka shillingi 10,000 ambayo ndo moja ya kumi kama akiba.

Hii yaweza kuonekana kidogo ila ukijijengea utaratibu wa kuweka kidogo kidogo baada ya mda utakuwa umeweka pesa nyingi kwani haba na haba hujaza kibaba.

SOMA ZAIDI:

  1. Uchambuzi Wa Kitabu Cha The Richest Man In Babylon
  2. MAKOSA 50 AMBAYO WATU HUFANYA KUHUSU FEDHA: Kosa La #2 Kukataa Kuchukua Hatua Kwa Kile Ambacho Unajua

Ni mimi ndugu yako
Godius Rweyongeza
kwa mawasiliano na ushauri
godiusrweyongeza1@gmail.com
0755848391.

Endelea kuitembelea blogu hii kwa makala zaidi za kuelimisha na kuhamasisha


One response to “Ijue Siri Ya Babiloni Kuwa Mji Tajiri Kuliko Yote Duniani”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X