Jinsi ya Kuepukana na Kauli Hizi Tatu (03) za Kukatisha Tamaa


Kwa kawaida mtu ukitaka kufanya jambo fulani la maana basi kila mmoja huwa anakuja na kauli zake na mtazamo wake.
Wako baadhi ambao hutoa kauli fulani ambazo hulenga kukukatisha tamaa ili usiendelee na kwa wengine kauli hizi, huwakatisha tamaa kweli na kuwafanya wasiweze kuendelea mbele kwelikweli.
Baadhi ya kauli hizo ni kama ifuatavyo.

1. Unapoteza muda.
Hawa husema hivi wakijua wewe hutaweza kufikia ndoto yako ambayo imo akilini mwako.

Ni muhimu kufahamu kwamba wewe ndiye uliye na maono na wewe ndiye mwenye uwezo wa kuona uendako. Hakuna mtu mwenye uwezo wa kuona kule ambako wewe unapaona. Usiwasikilize hao wewe songa mbele.
Hakikisha malengo yako umeyapanga  vizuri. Weka mpango wako na jinsi utakavyoukamilisha hatua kwa hatua

Anza sasa usisubiri mpaka pale utakapokuwa umejiandaa vizuri. Nakuhakikishia siku ambayo utakuja kusema nimejiandaa vizuri haipo. Kila siku utakuwa unaona bado kuna kitu fulani hujakamilisha na kuendlea kusema najiaandaa. Anza sasa. Kama hauko tayari sasa hutakuja kuwa tayari.

SOMA ZAIDI:  Usisubiri Mtu Yeyote Kuanza Kufanyia Kazi Ndoto Zako

2. Hilo huliwezi, fulani alifanya akashindwa.

Mtu wa aina hii anayekwambia kauli kama hiyo ni mwoga wa kufikria na mwoga wa changamoto.

Cha msingi ni kwamba kushindwa kwa fulani hakuwezi kukufanya na wewe kushindwa, yawezekana  alishindwa kukabiliana na changamoto na kuzitatua.
Kumbe kushindwa kwake kuwe chanzo cha wewe kufanikiwa. Fuatlia ujue ni nini yeye kilimfanya ashindwe, anza mara moja na uwe tayari kukabiliana na changamoto. Kadri utakavyoweza kutatua changamoto zaidi ndivyo utakavyokuwa katika hali nzuri ya kufikia mafanikio.

Ni muhimu sana kufahamu kwamba sio kila mtu anaweza kukushauri katika kile unachofanya. Mtafute mtu ambaye amewahi kufanya jambo fulani ambalo na wewe unataka kufanya ili aweze kukupa mwongozo juu ya jambo fulani. Nakuhakikishia huwezi kupoteza mda. Waache wao wapoteze mda kwa kukujadiri wewe. Songa mbele.

3.Haya mambo waachie wazungu.
Hii ni kauli nyingine ambayo watu hupenda kuitumia ilil kukukatisha tamaa. Mfano, nilipomwambia rafiki yangu kwamba nimeanzisha blogu alinijibu hivi  “  haya mambo ya kutengeneza na kuendesha blogu  waachie wazungu?”

Je, wewe kuna mtu amewahi kukwambia hivi?
Kiujumla mtu huyu naona anatawaliwa na utumwa akilini mwake, hali ambayo inamfanya yeye ajione hawezi kufanya jambo la maana isipokuwa wazungu tu.
Ebu jiulize swali hili  “ wazungu wana nini ambacho mimi sina kiasi kwamba baadhi ya mambo niwaachie wao ?”

Ni aibu kubwa sana kukuta mtu anatoa kauli kama hiyo. Hakuna jambo ambalo haliwezekani ukiamua. Kwa hiyo amua sasa akilini mwako kwamba nataka kufanya jambo fulani. Jiwekee utaratibu wa kujisemea na kujikumbusha na kufikria  kile ambacho kipo kwenye mpango wako kila siku.

Kwa uhakika kelele za kukatisha tamaa zipo kila kona, usiogope.amua sasa, anza sasa, wakati ni sasa, songambele

Najua kuwa ungependa kupata ushauri wa karibu zaidi moja moja kwa moja kutoka kwangu. Nitafute tuone ni lini nitakuwa na muda, ili nikupangie ratiba ya kuongea na wewe. Utalipia kiasi kidogo tu.

Saa moja ni laki moja mazungumzo kwa njia ya mtandao.

SAA MOJA NI LAKI MBILI NA NUSU MAZUNGUMZO YA ANA KWA ANA. Malipo yanafanyika kwanza, kisha unapewa tarehe (appointment) tutakapoweza kuongea

Tumia namba ya simu +255 755 848 391 kuwasiliana nami.

Makala hii imeandikwa na Godius Rweyongeza ambaye anaishi Morogoro nchini Tanzania.

Unaweza kujifunza zaidi kutoka kwa Godius Rweyongeza kupitia youtube channel yake hapa

Kwa ushauri niandikie songambele.smb@gmail.com

Kupata vitabu ambavyo ameandika Godius Rweyongeza, wasiliana naye kwa +255 684 408 755 na orodha ya vitabu vyenyewe unaweza kuiona HAPA. Chagua unachopenda, kisha twanga,  +255 684 408 755

Kujiunga na programu yetu ya uandishi. Wasiliana na +255 678 848 396

For Consultation only: +255 755 848 391  au godiusrweyongeza1@gmail.com

Ni rafiki na ndugu yako
Godius Rweyongeza
Tuwasiliane.
godiusrweyongeza1@gmail.com
0755848391

Endelea kusoma makala za kuelimisha na kuhamasisha kutoka kwenye blogu hii.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X