Kama Rasilimali Zipo Tatizo Ni Nini?


Habari za leo rafiki na ndugu msomaji wa blog ya SONGA MBELE imani yangu unaendelea vyema katika hatua ya kuelekea mafanikio. Karibu sana katika makala ya leo.Habari za kuhusu kuendelea na  kukua kwa uchumi wa Tanzania na Afrika kwa ujumla  ni jambo ambalo limekuwa linazungumziwa kwa muda mrefu sasa.

Wanasiasa, watalii, wanauchumi wasomi  na watu wengine wengi sana, wanakubaliana kwamba kuna rasilimali nyingi katika nchi hii ambazo zinatosha kuufanya uchumi wake uwe mkubwa na hawaoni sababu za kwa nini nchi hii iwe maskini.

Mpaka kuna makala moja kwenye gazeti la THE CITIZEN inayosema kwamba Mkoa wa Morogoro tu wa nchini Tanzania unatosha kuilisha Afrika nzima

Lakini wote kwa pamoja wamekubaliana kwamba kuna ssababu ambazo zinasababisha nchi hii iendelee kuwa maskini.
Baadhi ya hizo sababu ni kama
  • ukoloni mamboleo,
  • rushwa,
  • ufisadi,
  • ukoloni na utumwa ambao nchi za Afrika zimepitia,
  • watu wengi sana hawajaelimika,
  • imani za baadhi ya watu kwamba nchi za afrika zimelaaniwa,
  • kutokuwa na usawa katika soko la dunia,
  • uzembe,
  • ukosefu wa elimu yetu ya asili na sababu nyingine nyingi.
  • Kila sababu inaweza kuwa imebeba maana kubwa sana na haipaswi kubezwa lakini kitu cha msingi ni kila mtu kuondoa tatizo lake.
Soma zaidi hapa;
Sheria Muhimu Katika Kutengeneza Pesa Na kuwa TajiriJinsi Ya Kuondoka Kwenye Umasikini Wa Kipesa

.
Afrika inatoa somo kubwa sana kwa mtu kujua na kujitambua kwamba uwepo wa rasilimali haumaanishi kwamba utaishi maisha ambayo unayataka.
Tumesikia kuhusu ukosefu  wa maji katika maeneo ambayo yako karibu na mito,
Ukosefu wa chakula kwa watu wanaoishi na wanaomiliki ardhi yenye rutuba huku kukiwa na mvua za kutosha katika maeneo hayo.
Mambo yote hayo husikika katika nchi maskini. Je, unahitaji nini ili uweze kuzitumia rasilimali zako? Je, raslimali  zako ziko wapi? Je, unahitji nini ili uweze kuanza? Na unaanzaje? Haya ni maswali ambayo yamekuwa yakiulizwa na watu wengi sana.
Soma zaidi hapa;
   Jitafakari mwenyewe (wewe ni nani?)
Kujitafakari mwenyewe kwa umakini kunahitajika kama unahitaji kuwa na mwanzo mzuri wa kuanzia na kuzitumia rasilimali zilizokuzunguka. Unachohitaji kujiuliza  ni wewe uko kwenye hali gani sasa hivi?
Hili linaweza lisionekane ni jambo la muhimu la kufanya kwa sasa, lakini kama utajaribu utagundua mambo mengi na utapata kujijua mwenyewe na kufanya mabadiliko. Kumbuka huwezi kubadili kitu ambacho hukijui kabisa.


 Unataka kuwa nani?
Baada kujijua wewe ni nani unahitaji kwenda hatua moja zaidi. Jiulize wewe unataka kuwa nani? Unataka kwenda wapi?
Hali yako ya sasa itakufanya utafute maisha ambayo ni bora zaifi.

Angalia ni rasilimali gani zimekuzunguka?
Baada ya kujijua wewe ni nani na unataka kwenda wapi? Sasa ni muda wa wewe kuangalia ni kitu gani kipo kwenye mazingira yako ambacho wewe unaweza kukitumia kufika kule uendapo.
Majibu yote yapo kwenye mazingira yako. Je wewe una kipaji gani?
Una ujuzi gani?
Je ni kitu gani kinachoonekana ambacho unaweza kukitumia na kuanzia?
Je, ni huduma gani ambayo haitolewi mataani kwako?
Je ni huduma gani ambayo inatolewa kwa kiwango cha chini mtaani ambayo utaitoa kwa ubora zaidi?

Chukua hatua
Kiukweli sijui una umri gani na changamoto unazopitia ni zipi. Lakini hilo sio tatizo. Kitu cha msingi cha kufanya sasa hivi ni kuchukua hatua. Baadhi ya hatua ambazo utachukua hazitawafurahisha baadhi ya watu waliokuzunguka lakini kumbuka wewe ndiye dereva wa maisha yako.
SOMA ZAIDI: Huu Ndiyo Ustaraabu Wa Hali Ya Juu Ambao Unapaswa Kuwa Nao
Chukua hatua sasa badilika sasa na muda ni sasa na songambele
Endelea kusoma makala za kuelimisha na kuhamasisha kutoka kwenye blogu hii
Kujiunga na mfumo wetu wa kupokea makala maalimu kutoka SONGAMBELE BONYEZA NA UJAZE FOMU
 Ni mimi rafiki na ndugu yako
Godius Rweyongeza
Tuwasiliane
godiusrweyongeza1@gmail.com
0755848391
Asante


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X