Rafiki yangu wa ukweli, salaam. Hongera sana kwa kazi, siku ya leo, nataka kuongea na wewe kuhusu ustaraabu.
Mara nyingi watu huwa wanapenda kuonesha ustaraabu kwenye maeneo tofautitofauti. Ila leo hii ninataka nikwambie kuhusu ustaraabu wa hali ya juu ambao unapaswa kuwa nao.
Na aina hii ya ustaraabu ambayo unapaswa kuwa nayo ni kufanya kile unachopasawa kufanya.
Ndiyo, huu ndiyo ustaraabu wa hali ya juu kabisa.
Kama wewe ni mwimbaji, ustaraabu mkubwa sana ambao unaweza kuwa nao ni kuimba.
Kama wewe ni mwigizaji, ustaraabu mkubwa ambao unapaswa kuwa nao ni kuigiza.
Kama wewe ni mchoraji, ustaraabu wa wachoraji ni kuchora,
Ustaraabu wa waandishi ni kuandika
Ustaraabu wa dereva ni kuendesha kwa kufuata sheria za barabarani. Huo ndiyo ustaraabu pekee wa viwango vya juu.
Ukiwa na ustaraabu ambao unakuzuia wewe kufanya kazi unayopaswa kufanya, basi huo ustaraabu unanipa mashaka kidogo.
Hivyo basi siku ya leo nikusihi kitu kimoja tu. Anza kuwa mstaraabu. Sawa ee. Fanyia kazi yale unayopaswa kufanyia kazi bila ya kuchoka wala kurudi nyuma. Huu ndiyo ustaraabu pekee ambao unapaswa kuwa nao rafiki yangu.
Kama mpaka hapo umenielewa basi naomba unyooshe mkono juu.
Mpaka wakati mwingine.
SOMA ZAIDI
- Jinsi Ya Kushughulika Na Fedha Unazopata Kutokana Na Kipaji Chako
- Kama unafikiri elimu Ni ghali, jaribu ujinga
- JE, WAJUA KWAMBA DAKIKA KUMI NA TANO ZINAWEZA KUKUFUNDISHA LUGHA MPYA? DAKIKA 15 MTANDAO NI ZINAKUPA NINI?
Makala hii imeandikwa na Godius Rweyongeza ambaye anaishi Morogoro nchini Tanzania.
Unaweza kujifunza zaidi kutoka kwa Godius Rweyongeza kupitia youtube channel yake hapa
Kwa ushauri niandikie songambele.smb@gmail.com
Kupata vitabu ambavyo ameandika Godius Rweyongeza, wasiliana na +255 684 408 755
Kujiunga na programu yetu ya uandishi. Wasiliana na +255 678 848 396
For Consultation only: +255 755 848 391