Habari za leo rafiki na ndugu msomaji wa SONGA MBELE BLOG . Imani yangu unaendelea vyema katika hatua ya kutafuta na kuelekea mafanikio.Karibu sana katika makala yetu ya leo ambapo tunaenda kujifunza kitu kipya ambacho kitabadili mwelekeo wa maisha yetu
Kipaji ni kitu cha kipekee ambacho kimo ndani ya mtu. Hiki ni kitu ambacho mtu huzaliwa nacho na humtofautisha na watu wengine, hata kama wengine watakuwa na kipaji kile kile lakini kipaji cha mtu Fulani huwa na utofauti na humfanya wa pekee tofauti na wengine
Kipaji ni umahiri wa kipekee ambao mwenyezi Mungu ameweka ndani ya akili ya mtu unaoongoza usadifu wa viungo na fikra zake kufanya jambo kwa upekee kabisa.
Kipaji cha mtu kinatambulika kwa matendo yake na jitihada zake katika kufikiri na kujaribu mambo mbali mbalimbali. Maneno ya mwisho yana maana sana rafiki, naomba niyarudie tena jitihada zake katika kufikiri na kujaribu mambo mbalimbali.
Hatuwezi kujua kwamba wewe una kipaji cha kuimba mpaka pale utakapokuwa umejaribu kuimba, hatuwezi kujua kama wewe una kipaji cha kucheza mpira mpaka pale utakapokuwa umejaribu kucheza mpira, hatuwezi kujua kama wewe una kipaji cha kuongea mpaka pale utakapojaribu kuongea.
Siku zote kipaji kimo ndani ya mtu kikisubiri kufufuliwa, kwa hiyo ni muhimu sana kujua kipaji chako ni kipi ili kukiinua na kukiuza zaidi.
Soma zaidi hapa: Hadhi ni nini?
Namna ya kutambua kipaji chako.
Kila mmoja wetu ana kipaji, ingawa mara nyingi sio wote tunaopata nafasi ya kuvitambua vipaji vyetu na kuvifanyia kazi. Hii inatokana na jamii yetu kutovipa nafasi vipaji vyetu katika kuvifufua kuviendeleza na kuvikuza.
Hizi hapa ni njia ambazounaweza kutimia kutambua kipaji chako
1. Vitu gani unapendelea ulikuwa unapendelea ulipokuwa mtoto?
Vipaji vya mtu vinaanza kujionesha mapema akiwa motto. Ulipokuwa mtoto kuna vitu ulikuwa unapendelea kufuatilia na kuvifanya. Hata kwenye michezo na wenzako kuna michezo ambayo ulikuwa unaifurahia sana kuliko mingine. Kuna michezo mingine isingechezwa bila ya wewe kuwepo.
Je unaikumbuka hiyo rafiki?
Kama hukumbuki kaa uyatafakari maisha ya utotoni. Waulizie wazazi, walezi, ndugu wako wa karibu ambao walikuwa wanakuona wakati unakua. Kumbuka ni mambo gani ulikuwa unapendelea ulipokuwa shuleni. Je, ni vitu gani ulikuwa unangara ulipokuwa shuleni?
Soma zaidi hapa; Matendo Hutibu Uoga
2. Vitu gani unapendelea sasa hivi?
Angalia wakati uliopo kwa sasa, ukiangalia maisha yako vizuri utagundua kwamba kwa sasa kuna vitu unapendelea kufuatilia kwa undani. Angalia vitu ambavyo unavijua, unavifanya na unavifurahia zaidi.
Je watu wanakufuata na kukuomba ushauri katika mambo gani?
Je kitu gani ambacho watu wanaelekezwa kwako ili uwasaidie wanapokuwa na shida?
Je ni kitu gani ambacho watu wakishindwa lazima wakufuate ili uwasaidie?
Je umevijua ni vitu gani? Basi hivi ndio vitu ambavyo uko vizuri na watu wameridhishwa na utendaji wako. Ebu vipe thamani zaidi rafiki?
3. Ni vitu gani upo tayari kufanya hata kama hulipwi?
Kuna vitu ambavyo ukiona mtu anafanya ila havifanyi kwa ubora basi utakuwa tayari kumwambia na kumwelekeza ili aweze kuvifanya kwa weredi mzuri sana. Hivi navyo ni sehemu ya vipaji vyako.
Naamini katika kila hatua kuna vipaji utakuwa umegundua rafiki. Chagua ambavyo utaanza kuvifanyia kazi sasa.
Nakutakia utekelezaji mwema
Badilika sasa
Anza sasa
Muda ni sasa
Ili upate makala maalumu kutoka songambele blogu BONYEZA HAPA ILI KUJIUNGA
Endelea kusoma makala za kuelimisha kutoka kwenye blogu hii
Ili upate makala maalumu kutoka songambele blogu BONYEZA HAPA ILI KUJIUNGA
Ni mimi rafiki na ndugu yako
Godius Rweyongeza
Tuwasiliane
godiusrweyongeza1@gmail.com
Asante.
7 responses to “Kipaji Ni Nini?”
Unajua kwamba kila binadamu anazaliwa na vipawa na vipaji 500-700. Haha new challenge bro
Unajua kwamba kila binadamu anazaliwa na vipawa na vipaji 500-700. Haha new challenge bro
Naam
[…] Hakikisha unasoma: Kipaji Ni Nini? […]
[…] Walau siyo mara yako kusikia kuwa binadamu wote ni sawa. Au kusikia haki sawa kwa wote. Japo kuna huo usawa kwa watu wote, linapokuja suala zima la kipaji na uwezo mkubwa tulionao tunatofautiana. […]
Kipaji ni kama jiwe la thamani na humfaa mtu kila ageukapo.
Mithali 17:8
[…] Kipaji Ni Nini? […]