KIPAJI NI DHAHABU-1 binadamu wote ni sawa ila uwezo ni tofauti


Walau siyo mara yako kusikia kuwa binadamu wote ni sawa. Au kusikia haki sawa kwa wote. Japo kuna huo usawa kwa watu wote,  linapokuja suala zima la kipaji na  uwezo mkubwa tulionao tunatofautiana.

Ndio maana kuna watu wanajulikana kama multi-talented. Wana uwezo katika maeneo tofauti tofauti na wanaweza kuyafanyia kazi hayo maeneo kwa ustadi.

Diamond uwezo wake upo kwenye kuimba au basi tuseme Diamond kipaji chake ni kuimba. Samatta kipaji chake ni kucheza mpira.
Shigongo kipaji chake ni kutunga hadithi tamu, wewe pia unapaswa kugundua kipaji chako.

Una uwezo mkubwa ndani yako ambao hujaanza kuutumia. Thomas Edison aliwahi kunukuliwa akisema kwamba, laiti kama tungeutumia uwezo mkubwa tulionao Kama inavyostahili, sisi wenyewe tungejishangaza kwa matokeo ambayo tungepata”

Uwezo wako ni mkubwa kiasi kwamba kama ungeishi miaka elfu moja bado usingeweza kuutumia ukaisha.

Kipaji huwa hakitumiwi kikaisha. Badala yake kadiri unavyokuwa unakitumia ndivyo kinakuwa kinazidi kuimarika zaidi.

Wewe unafahamu kipaji chako?
Pata ebook ya kipaji ni dhahabu kwa gharama ya elfu tano tu (5,000/-).


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X