Vitu Vitano Ambavyo Vitakuweka Huru Kiuchumi Ndani Ya 2018


Unaweza kuishi kqa siku ngapi kama mshahara wako utasitishwa leo? Unaweza kwenda hatua ngapi MBELE yako kama biashara yako itaanguka leo?
Kitu kimoja na cha muhimu sana ambacho kila mwanadamu anakihitaji hapa duniani ni Uhuru. Wengi sana wamesema kwamba tumezaliwa huru. Sawa na Mimi nakubalina na hilo. Wengine wanasema binadamu wote ni huru na sawa, yaani wakimaanisha kwamba binadamu wote wanaishi chini ya ile sheria yetu vijana tunayoiita fifite fifite (50/50). Au hamsini kwa hamsini.

Kila mtu yupo sahihi kwa upande wake ila ukweli ni kwamba kuna maeneo mengi sana ambayo binadamu hawajawahi kuwa sawa hata siku moja. Yaani haijawahi kuwa hamsini kwa hamsini. Na eneo mojawapo ni eneo la PESA. Watu wawili wameajiriwa kwenye kampuni moja, na pengine wanafanya kazi ileile lakini mshahara wao haulingani!!!
Watu wawili wanamshahara sawa ila maisha yao sio sawa sawia. Mmoja anaishi maisha ya furaha na utajiri. Mwingine umaskini unamwandama.
Watu wawili wanafanya kazi kampuni moja, mmoja analipwa kiwango cha juu sana japo kazi yake ni ndogo na mwingine analipwa kidogo japo kazi yake ni kubwa sana.

Kutokana na hali hizi hapa basi kunahitajika mpango binafsi, tena mpango madhubuti wa kukuwezesha wewe hapo kupiga hatua kubwa sana. Mpango huku utauweka wewe mwenyewe na utakuwezeha wewe kuweza kupiga hatua kubwa sana. Leo hii nimekuandalia mambo matano ambayo kama utayafanya ndani ya mwaka 2018 basi utaweza kuwa huru kiuchuni walau kwa miezi mitatu mpaka sita.
Isome vizuri na uifanyie kazi.

1. JILIPE MWENYEWE KWANZA

Unaingiza shilingi ngapi kwa siku kwa wiki, kwa mwezi? Hakikisha kila senti inayoingia katika mfuko wako unatoa asilimia 10 ya akiba. Hii ni kanumi ya mafanikio popote pale duniani. Hii ndio kusema kwamba kama mshahara wako ni 100,000 basi huna budi kutoa elfu kumi kama akiba. Itumie hii kwa kila pesa ambayo inakuja mkononi mwako.

Soma Zaidi; Ijue Siri Ya Babiloni Kuwa Mji Tajiri Duniani

2. USITUMIE ZAIDI YA MAPATO YAKO
2018 ni mwaka ambao unapaswa kupiga hatua kubwa sana. Na huwezi kuruka kufika eneo fulani kama haupo tayari kuinama kidogo. Kiufupi ni kwamba huwezi kuwa komando kwa kufanya mazoezi ya mgambo. Ndani ya mwaka huu wa 2018 hakikisha unapiga mazoezi ya kikomando. Moja, ya zoezi hilo la kikomando ni kutumia kiasi kidogo zaidi ya kipato chako. Kama kipato chako ni elfu kumi na matumizi yako ni elfu kumi na mia moja basi jua kwamba upo katika njia ya umasikini ndani ya mwaka. 2018. Lakini kama kipato chako ni elfu kumi na unatumia elfu tisa mia tisa, basi jua kwamba  upo katika njia ya utajiri.
 Kanuni moja muhimu sana ambayo inaiongoza dunia na watu wote waliofikia mafanikio makubwa kiuchumi ni kutumia kidogo zaidi ya kile wanachoingiza.

3. PUNGUZA MATUMIZI YASIYO YA LAZIMA
Siku zote matumizi unayoyafanya tunawwza kuyaweka kwenye maeneo mawili. Matumizi ya lazima (comfort). Na matumizi yasiyo ya lazima (luxury). Kwa hiyo utumie mwezi mmoja mwaka huu kufanya utafiti.
Ndani ya mwezi huu andika kila pesa inayoingia na inayotoka. Chukua dafatari na uligawe kwenye maeneno mawili. Eneo la kwanza matumizi ya lazima, na eneo la Pili matumizi yasiyo ya lazima. Endelea kuandika hata kama kazi itaonekana ni ngumu sana. Iambie akili yako ni kwa mwezi mmoja tu. Usitumie zaidi ya unavyoingiza ndani ya 2018.

3. USIFANYE ILI KUWAEIDHISHA WENGINE.
kuna jamaa mmoja alikuwa ana Rafiki yake.  Rafiki yake huyo alikjwa na maisha mazuri kiuchumi. Ana gari, nyumba nzuri, mke na watoto. Yule jamaa akajiambia huyu Rafiki yangu kuna kipindi tulikuwa na kipato sawa, ila sasa amepiga hatua. Ngoja nitamwonesha kwamba na Mimi nimo. Akaenda kukodi gari ili rafiki yake atakapopita njia yake na yeye apite njia ile ile. Alitaka kumwonesha rafiki yake kwamba  na hawajazidiana.

Rafiki yangu kosa kubwa sana ambalo unaweza kulifanya maishami mwako ni kujionesha kwamba una kitu, wakati huna. Ni kufanya matumizi makubwa sana wakati kiasi ukichonacho hakiruhusu. Epukana na kosa hilo mwaka huu 2018. Usiende bar na kuwanunulia watu bia, soda kuta ila vichache ili uonekane kwamba una pesa.

Soma zaidi; Nani anakujua?

4.  JALI SANA AFYA YAKO
mwaka 2018 afya yako inapaswa kuwa kipaumbele kikubwa sana. Hakikisha kila mara unafanya mambo yatakayoiimarisha afya yako. Hajawahi kufanikiwa mtu akiwa kitandani. Kwa hiyo kula kwako, kunywa kwako kutembea n.k kuwe ni kwa ajili ya kujali afya.
Ni bora kunywa glasi moja ya maji ndani ya 2018 kuliko kunywa chupa nzima ya soda.
Ni bora kutembea maili moja ndani ya 2018 kuliko safari ya maili elfu kwenye kochi. Afya yako ni muhimu sana ndani ya 2018.

5. USITABIRIKE
Moja ya kosa linalofanywa na watu walio wengi, hasa wale walio ajirani ni kutabirika. Pale mshahara wake unapoingia kila mtu anajua. Hivyo kujikuta anakaribisha mikono ya watu wengi wanaoomba msaada. Mwaka 2018 usitabirike. Hakuna mtu anayepaswa kujua kwamba sasa una pesa. Maisha yako yawe yale yale unapokuwa na pesa na unapokuwa huna. Kama pesa inapoingia tu kila mtu anajua basi jua kwamba unahitaji kujirekebisha ndani ya mwaka huu 2018.

Tukutane kileleni disemba 2018
Ulikuwa nami,
Godius Rweyongeza
($ongambele)
0755848391
www.songambeleblog.blogspot.com

,

2 responses to “Vitu Vitano Ambavyo Vitakuweka Huru Kiuchumi Ndani Ya 2018”

  1. Asante kaka godius nilikuwa sijawahi kuingia kwenye blog hii lakini Leo nilivyoingia nimekutana na mondo ambazo zitanisaidia kufikia malengo yango katika mwaka huu 2018,asante kwa msaada wako wa elimu hii unayotupatia

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X