UCHAMBUZI WA KITABU CHA WEALTH OF NATIONS-2


Ukurasa wa 27-37

Utajiri Wa Mataifa

“Katika miaka ya zamani, tunakuta kwamba vitu vilipewa thamani kulingana na idadi ya ng’ombe, mfano silaha ya kujikinga wakati wa vita (armour) iliyokuwa inatoka maeneo ya Diomede, ilikuwa sawa na ng’ombe tisa. Wakati silaha hiyo hiyo kutoka maeneo ya Glaucus ilikuwa ni sawa na ng’ombe mia.

Chumvi ilikuwa ni chanzo cha mabadilishano huko Abyssinia
Magamba nayo yalikuwa chanzo cha mabadilishamo huko India
Tumbaku ilitumika Virginia na nguo zilitumika kwenye maeneo mengine kama chombo cha mabadilishano.”

Lakini kati ya vitu vyote hivyo vilivyokuwa vikitumika kubadilishana, chuma ndicho kilionekana kitu cha kipekee sana kwenye mabadilishano. Na hivyo chuma kilitumika sana.

Hata hivyo kama ingetokea kwamba mtu hana chuma, na badala yake ana ng’ombe, basi ingempasa kuchukua ngombe ili apate anachohitaji, labda chumvi.

Hata hivyo kwa ubadilishaji huu mtu alikuwa analazimika kutoa ng’ombe mzima mzima ili kupata chumvi kidogo maana asingeweza kumgawa ng’ombe kwa namna yoyote ile. Na kama angetaka chumvi zaidi alipaswa kuongeza idadi ya ng’ombe zaidi ili apate chumvi.

Njia hii ilikuwa inapunja, lakini hata hivyo hakukuwa na jinsi maana ndio njia pekee iliyokuwepo.
Kama mtu angekuwa na chuma   na ikatokea anahitaji chumvi kidogo, basi ingekuwa rahisi kwake kukata chuma ili kiasi cha chumvi kiendane na ukubwa wa chuma.

Hata hivyo japo kulikuwa na uwezo na kukata vyuma hivi, lakini bado hakukuwa na kipimo kizuri cha kukata vyuma hivi, hivyo kufanya baadhi ya vyuma kuwa vikubwa na vingine vidogo.
Lakini pia vyuma havikuwa na nembo yoyote ile.

Ndipo kwa mara ya kwanza serikali ya Roma iliweka watu maalumu wa kukata na kuhakikisha kila chuma, kinachotumika kwenye mabadilishano kinakuwa na ukubwa sawa na kingine. Na hivyo kwa mara ya kwanza kabisa katika dunia kukazaliwa TAASISI ZA PESA.

Hata hivyo pesa hizi bado zilionekana kuwa na thamani tofauti.
Pesa iliyotengenezwa kwa dhahabu ilikuwa na thamani tofauti na pesa iliyotengenezwa kwa shaba lakini pia pesa iliyotengenezwa kwa chuma nayo ina thamani tofauti kabisa.

Sasa THAMANI ni nini?
Thamani tunaweza kuiangalia katika namna mbili tofauti.
Mosi, tunasema thamani katika matumizi (value in use)
Thamani katika  mabadilishano (value in exchange)

Kuna vitu unakuta vina matumizi makubwa ila havina  thamani kubwa na vitu vyenye thamani kubwa, havina matumizi makubwa.
Mfano maji yana matumizi makubwa ila hayana thamani kubwa na dhahabu ina matumizi madogo, ila thamani kubwa.

Kabla sijamalizia uchambuzi wa leo naomba nikwambie kitu kimoja. Mabadilishano haya ndio yametufikisha kwenye uwepo wa pesa za sasa tunazoziita, shilingi, rand, dola, poundi, euro na nyinginezo.

Lakini kwa sasa tunashuhudia pesa hizi zikishuka na kupanda thamani kila iitwayo leo.

Sasa ni nini hiki kinafanya pesa ipande au kushuka thamani?

Endelea kufuatilia chambuzi hizi.
Siku zijazo nitakuwa nikidokeza kitu gani kinafanya pesa ipande na kushuka thamani.

Soma Zaidi Uchambuzi Wa Kitabu: WEALTH OF NATIONS-1

ANGALIA VIDEO HII:  CHUMA HUNOA CHUMA
Ndimi,
Godius Rweyongeza
0755848391

KUPATA KITABU CHA KUTOKA SIFURI MPAKA KILELENI BONYEZA HAPA


HUDUMA NYINGINE UNAZOWEZA KUPATA KWANGU HIZI HAPA

KUPATA MAKALA MAALUM KWA WATU MAALUM KILA WIKI BONYEZA HAPA

,

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X