Naandika makala hii ikiwa ni usiku saa 2 kasoro dakika tatu sasa ya tarehe 21//2/2020. sijajua wewe makala hii unaisoma muda gani na siku gani. Nimeamua niandike makala hii baada ya kuwa nimetoka kufanya mauzo sehemu. Hivyo wakati narudi njiani ndio nikakumbuka kauli mojawapo ya Tony Robins. Hivyo nikaona wazi kwamba kuna somo kubwa sana la kujifunza hapa. na nimeamua nikushirikishe somo hili hapa, ili na wewe uweze kujifunza kitu na kuchukua hatua mara moja.
Tony Robins alianza maisha yake uhamasishaji kwa kuuza kazi za Jim Rohn. Alikuwa anauza CDs, vitabu na mafunzo mengine ya Jim Rohn. Sasa wakati anawazungukia watu na kuwauzia mafunzo hayo. Tony Robins alikuwa na kauli yake maarufu sana. Alipokuwa anaenda kwa mtu na yule mtu akawa haeleweki kwenye kununua, basi Tony Robins alikuwa anamwambia, NIKATALIE ILI NIKALIPWE. Sasa watu walikuwa wanashangaa, yaani wewe unalipwaje mimi nikikutalia. Tony Robins akawa anawaambia kwamba mnikatalia watu 10 anatokea mtu mmoja ambaye anafanya manunuzi makubwa. Wakikataaa wengine 10 anatokea mtu mwingine mmoja ambaye ananunua. Na anafanya manunuzi makubwa.
Kitu kingine kikawa ni kwamba wakikataa watu mapema basi inakuwa ni nafasi yake kuwahi kuwaendea watu wengine ambao watanunua.
Sasa leo ambacho ninataka tujifunze sio kwamba na wewe uende uanze kuwaambia watu hicho kitu. Bali kwamba ukienda kuuza kitu kwa mtu na akawa hajanunua basi sio kwamba huo unapaswa kuwa mwisho wako. Wewe endelea mbele bila kukosa. Endelea mbele. Kadri utakavyokuwa unawafikia watu zaidi ndivyo unakuwa na nafasi kubwa zaidi ya kuuza. Kuliko pale unapokuwa umewafikia watu wachache tu.
Rafiki yangu naomba uuchukue kitu hiki muhimu sana kwenye kazi zako ambazo unafanya. Kwenye biashara yako na hata kwenye mauzo. Jitahidi kwamba uwafikie watu wengi zaidi.
Nilichogundua unapokuwa unauza kitu. Kuna watu ambao wakikuona tu watajenga fikra za kukitaa kitu chako kabla hata hawajakusikiliza.
Kuna watu ambao watakusililiza ila hawatanunua.
Kuna watu watakusililiza na hata kabla hujamaliza wataomba kununua.
Na kuna watu watakusiliza ila kama hutawaambia wanunue, hawatanunua. Hivyo jitahidi unapoamua kufanya mauzo basi unamwangalia mtu wako uliyemlenga vizuri.
Ukiona mtu ameshawishika na yupo tayari kununua, basi usiendelee kuweka maneo mengi zaidi. Badala yake, mpe bidhaa na yeye akupe fedha.
Ukiona kwamba mtu mpaka anahitaji aambiwe kwamba nunua au chukua bidhaa hii. Basi mwambie hivyo. Rafiki yangu hayo ni mambo ya muhimu sana ambayo niliona nikwambie siku ya leo.
Nashukuru sana. Na ninakutakia kila la kheri.
Naweka kalamu chini ikiwa ni saa 8 dakika 13 sasa usiku.
Kila la kheri.
Soma Zaidi: Vitu Vitano Vinavyoharibu Ubunifu Wa Watanzania
kijana usidanganyike, wakati unazidi kusogea
Ni mimi anayejali mafanikio yako
GODIUS RWEYONGEZA
KUWA MIONGONI MWA WATU AMBAO WANAPOKEA MAKALA MAALUMU KWA WATU MAALUMU KWA KUBONYEZA HAPA