Ushauri Muhimu Kwa Mtu Anayeanza Biashara Kutoka Jack Ma


Rafiki yangu, hongera sana kwa siku hii ya kipekee sana. Bila shaka umeianza siku yako vyema kabisa. siku ya leo nakuja kwako na ushauri muhimu kwako wewe ambaye unapenda kuanzisha biashara. Ushauri huunimeona niulete kutoka moja kwa moja kwa Bilionea wa China, Jack Ma. Nimemleta kwako Bilionea huyu kwa sababu kanuni kuu za mafanikio ni zile zile. Haijalishi uko China, haijalishi upo Afrika au Ulaya. Siku zote kanuni huwa inabaki kuwa kanuni.
Nadhani mfano mzuri wa kanuni ambayo huwa haibadiliki ni kanuni ya uvutano. Haijalishi upo Marekani, ukirusha jiwe juu litarudi chini. Ukienda Ulaya ukarusha jiwe juu, lazima tu litarudi chini. Na bado ukirudi hapa kwetu Tanzania ukarusha jiwe juu, litarudi chini pia. Kitu hiki ndio kimenisukuma nimlete kwako Bilionea wa kichina Jack Ma, ili siku ya leo aweze kuwasilisha kwako mambo matano muhimu ya kuzingatia kwako wewe unayetaka kuanzisha biashara.
KABLA HUJAANZA KUSOMA JACKA MA hakikisha kwamba umejiunga na mfumo wetu wa kupokea makala maalumu kwa watu maalum.  Kama hujajiunga unakosa mengi sana. BONYEZA HAPA MARA MOJA.
KWANZA UNAPASWA KUWA MVUMILIVU
Biashara sio mchezo wa kubahatisha kwamba unacheza mchana jioni unashinda. Ni kitu kikubwa ambacho unahitaji kuwekeza muda wako, nguvu zako, akili na fedha. Sasa hivi vitu vyote sio vitu ambavyo utaweza kuvifanya ndani ya siku moja tu na kufanikiwa. 
Na pengine kitu ambacho umeanzisha kinaweza kisilete matunda haraka kadri unavyotegemea. Kitu hiki hapa ndicho kinamsukuma Jack Ma kukwambia kwamba unapaswa kuwa mvumilivu. Bila shaka lolote Jack Ma ameenda kwenye nyayo zilezile za wahenga wetu waliotuambia kwamba mvumilivu hula mbivu. Kwa hiyo na wewe kuwa mvumilivu, unapoanzisha biashara.
Usikate tamaa mwanzoni mwa biashara kabisa. usikate tamaa kwa sababu umeona kwamba mwanzoni wateja hawajatokea kwa wingi kama ulivyokuwa unatarajia. Usikate tamaa kwa kuona kwamba wale watu waliokuwa wanakwambia kwamba watakuja kwako kununua bidhaa zako hawajaja. Badala yake wewe songambele bila kurudi nyuma, muda wowote na wakati wowote. Wewe endelea tu kusongambele.
PILI KUWA NA WATU SAHIHI KWENYE KUFANYA KAZI
Rafiki yangu, Jacka Ma anasema kwamba,huhitaji kuwa mtu bora duniani. Wala huhitaji kukaa na watu bora sana duniani. Ila unahitaji kuwa na watu sahihi. Watu wanaoamini kwenye ndotoyako na hiyo biashara yako. Unaaweza ukawa umeanza  biashara kwa namna ya udogo  ila wewe ukawa unaona mbali sana na hiyo biashara yako ambayo unayo sasa hivi.
kwa hiyo siku zote hakikisha kwamba unakuwa na watu sahihi ambao unatembea nao kuelekea ndoto zako kubwa.
Epuka kuwa na wakatisha tamaa.
Epuka kuwa na watu ambao wanakupunguzia nguvu zako
Epuka kuwa na watu ambao wanakurudisha nyuma
Epuka kuwa na watu ambao kila mara wanataka kuona umeanguka chini.
USITAKE KUJUA NI KUJUA NI KITU GANI AMBACHO UNAENDA KUPATA. JIULIZE NI KITU GANI AMBACHO WEWE UNAENDA KUTOA
Hiki kitu ndio kimekuwa kinawakwamisha vijana walio wengi. kila mara  akitaka kufanya kitu au akiitwa kufanya kitu anaanza kujiuliza nitapata nini. akiona kwamba maslahi ya muda mfupi hayalipi basi anaachana na hicho kitu. Jacka Ma anasema kwamba usikimbilie kuuliza kile ambacho utapata. Badala yake jiulize ni kitu gani ambacho wewe unaenda kutoa kwa hao watu. Ni kwa msingi huu huu Zig Ziglar aliwahi kusema kwamba, ‘unaweza kupata kitu chochote kile ambacho unataka, kama utawasaidia iwatu kiasi cha kutosha kupata kile ambacho wao wanataka’. Kwa hiyo wewe kijana tafuta kujua ni kitu gani unaweza kutoa kwa watu kuwasaidia kwanza, usiulize ni kitu gani nitapata mimi kwanza.
LENGA MBALI ZAIDI
Jack Ma anasema kwamba haupaswi kuwa na malengo ya  wiki au mwaka mmoja. Anasema kwamba unapaswa kuwa na malengo ya miaka 10 ijayo. Jacka Ma anasema kama hauna malengo ya muda ila unashutukiza tu kwa kuwa na malengo ya muda mfupi, basi malengo haya ya muda mfupi yatakupoteza na muda mwingine yatakufanya upoteze mwelekeo. Hivyo basi anasisitiza sana uweke uwe na malengo ya muda mrefu maishani mwako.
USIKIMBIZANE NA  MATUKIO YA SASA HIVI
Jack Ma anasema kwamba haupaswi kukimbizana na matukio makubwa ambayo yanaendelea kwa sasa. badala yake wekeza nguvu na juhudi kubwa kwa ajili ya miaka 10 au 20 ijayo. Kile kitu ambacho kila mtu anakimbizana nacho kwa sasa hivi, kinaweza kisiwe kitu sahihi kwako.
Wewe unapaswa kuwa na sababu ambazo zitakufanya wewe uendelee kuwepo kwa kishindo kikubwa miaka 10 ijayo. Na sio kuweka nguvu kwenye vitu ambavyo vinabadilika kila siku.
USISUBIRI KILA KITU KIKAE SAWA KWA AJILI YAKO
Usisubiri kila kitu kiwe sawa kwa ajili yako. Usisubiri sheria zote zipangwe vizuri kwa ajili yako. Pale ambapo kila kitu kinakuwa kimekaa sawa basi kunakuwa hakuna nafasi tena kwa ajili yako. Unapaswa kuchukua hatua haraka kabla hata serikali haijafikiria hicho kitu, kiasi kwamba serikali ikija kusema kwamba kila kitu sasa kimekaa sawa. Wewe utakuwa umeshaanza safari yako kuelekea eneo jingine.

Rafiki yangu huo ndio ushauri muhimu sana kutoka kwa Jack. Ambaye ni Bilionea wa kichina.  Bila shaka umejifunza kitu ambacho unaenda kufanyia kazi mara moja. sasa naomba uingie YOUTUBE mara moja ili uweze kuangalia SOMO  hili muhimu kkuhusu JINSI YA KUTENGENEZA FEDHA MTANDAONI wewe mweyewe utalipenda. Ukimaliza SUBSCRIBE kwa ajili ya mafunzo zaidi yatakayokuwa yanakuja.
Ni mimi anayejali mafanikio yako
GODIUS RWEYONGEZA

KUWA MIONGONI MWA WATU AMBAO WANAPOKEA MAKALA MAALUMU KWA WATU MAALUMU KWA KUBONYEZA HAPA

SUBSCRIBE KWENYE CHANNEL YANGU YA YOUTUBE HAPA


JIUNGE NAMI KWENYE NURU ANGAZA

, ,

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X