Kama kuna shida ambayo inawakabili vijana walio wengi kwenye ulimwengu wa leo basi ni kitu kinachoitwa mtaji. Mtaji limekuwa ni tatizo kubwa sana kwa vijana wengi na hata watu wazima, hata hivyo nipende kusema kwamba hakuna sifa yoyote kwenye kutokuwa na mtaji.
Kuna watu ambao kila mwaka wanalalamika kwamba hawana mtaji, unaweza kukuta kwamba mtu alikuwa analalamika mwaka 2010 kuwa hana mtaji, mwaka 2015 pia alikuwa analalamika na mwaka 2020 bado alikuwa analalamika kuwa hana mtaji na bado ataendelea kulalamika mwaka 2025. Kwa nini, kwa sababu kulalamika kwamba hauna mtaji ni rahisi sana kuliko kujitoa kwa vitendo kuutafuta huo mtaji.
Kwenye andiko hili ninaenda kukuonesha ni kwa namna gani ambavyo unaweza kuupata mtaji, na ubora mitaji ninayoizungumzia kwenye andiko hili tayari unayo ila tu unaipuuzia, au unaitumia ila sasa hujajua namna ya kuitumia vizuri zaidi kwa manufaa, na hiki ndiyo kitu ambacho ninaenda kueleza.
Hadithi Ya Mtu Aliyeuza Shamba La Alamsi Kwenda Kutafuta Almasi
Ujue nikikwambia kwamba tayari mtaji unao unaweza kuona kama vile ni kitu cha ajabu sana, na pengine unaweza kuamua kupuuzia kusoma andiko lililobaki. Binafsi sikulazimishi, ila walau ningependa kukuhakikishia kuwa asilimia kubwa ya mtaji unaouhitaji tayari unao.
Kabla sijakwambia mitaji hiyo ningependa nikudokeze kidogo hadithi ya mtu ambaye aliishi miaka mingi iliyopita. Mtu huyu alikuwa anaishi maisha mzuri na hakuwa na shida wala kitu chochote kinachomsumbua. Labda alikuwa na changamoto kama ambavyo mimi na wewe tunakutana nazo kila siku.
Siku moja mtu huyu alitembelewa na mchungaji ambaye alimwambia kwamba ukiwa na almasi inayolingana na kidole chako tu, unaweza kuimiliki dunia nzima. Baada ya mazungumzo hayo mchungaji aliondoka na kwenda nyumbani kwake. Huku yule bwana ambaye alijulikana kama Ali Hafed akiwaza namna ambavyo angeweza kupata almasi iliyolingana na kidole chake tu. Kesho yake bwana Ali Hafed aliuza mali zake na shamba lake, kisha aliikabidhi familia yake kwa jirani yake na kuondoka kwenda kusikojulikana ili kuitafuta almasi. Alianza kuzunguka huku na kule ili kuipata almasi lakini baada ya muda mwingi wa mahangaiko bila kupata chochote fedha yake iliisha, alipata mfadhaiko na hata kuchoka. Baadaye, mtu huyu alikutwa amekufa kandokando ya mto Barcelona nchini Hispania.
Huku nyumbani kwake alipotoka, shamba lake lilichukuliwa na bwana mpya ambaye siku moja wakati ananywesha mifugo wake aliona jiwe lililompendeza sana kutokana na mg’ao wake. Hivyo aliamua kuondoka na hilo jiwe mpaka kwake. Nyumbani kwake aliliweka hilo jiwe eneo la wazi tu.
Ingekuwa siku hizi basi tungesema kwamba aliliweka mezani (sebuleni). Sasa ikawa imetokea tena yule mchungaji akawa anapita kwenye lile eneo, alipofika kwa yule jamaa aliyechukua shamba la Ali Hafed alishangaa kuona jiwe ambalo moja kwa moja alilitambua kama almasi, pale pale kwa sauti ya mshangao aliuliza, Ali Hafed karudi?!
Aliambiwa hapana. Kwa nini unauliza hivyo. Alisema “hii ni alamasi na mimi nikiiona naitambua tu” alisema hivyo huku akionesha kidole chake kwenye jiwe alilokuwa amebeba yule bwana kutoka kule shambani. Kumbe loo, bwana Ali Hafed alikuwa ameuza shamba la almasi kwenda kutafuta almasi kusikojulikana.
Inawezekana bwana Al Hafed alikuwa analalamika mara nyingi sana kwamba hana mtaji, maisha magumu, vyuma vimekaza na maneno mengine ya aina hiyo wakati akiwa amelalia mtaji mkubwa. Unadhani huyu bwana alikuwa anahitaji mtaji wa fedha?
Walau kwa hilo tutakubaliana kuwa huyu jamaa alikuwa haitaji mtaji fedha maana alikuwa tayari amezungukwa na almasi za kutosha. Sasa alikuwa anahitaji nini? Ukiniuliza mimi nitakwambia kwamba kilichohitajika kwake ilikuwa ni kufunguliwa tu kiakili. Alihitaji kupata maarifa sahihi ambayo yangemwezesha kujua almasi inafananje tu. Kwa sababu kutokana na hadithi hii tunaona kwamba huyu bwana japo alizunguka kutafuta almasi, ila alikuwa haijui. Laiti angekuwa anajua almasi inavyofanana, asingeuza shamba lake.
Na hiki kitu tunakiona kwenye jamii yetu. Unaweza kukuta mtu analalamika kwamba anataka mtaji, lakini muulize kwamba wewe unataka mtaji wa shilingi ngapi na ukiupata utaufanyia nini? Hapo ndipo mtu ataanza kujiuma uma. Sasa mtu wa aina hiyo si sawa na Al Hafed tu!
Inawezekana bwana Al Hafed aliipita almasi nyingi tu njiani kwenye kuzunguka kwake, lakini kwa sababu tu alikuwa haijui bado aliendelea kuitafuta. Yaani, kama kukimbiza upepo basi huyu bwana alikuwa anakimbiza upepo kweli!
Na hapa ebu mfikirie mtu ambaye hajui kiwango gani cha mtaji anataka wala hajui anataka fanye nini. ataendelea kulalamika tu kwamba hana mtaji, wakati labda mtaji wake aliokuwa anahitaji ni simu yake tu.
Dhana Potofu Kuhusu Mtaji
Moja ya dhana iliyopo kuhusu mtaji ni kwamba, mtaji ni inapaswa kuwa fedha nyingi sana. kwa hiyo kuna watu ambao wanakuwa wanafikiria kwamba ukizungumzia mtaji unakuwa unaongelea mamilioni ya fedha. Labda milioni 50. Kwa wengi ukiongea kwamba nina milioni 200, hapo sasa ndipo watafahamu kuwa kweli una mtaji ila ukiwaambia kwamba una elfu 50, wataona kama masihala vile.
Labda kitu kimoja kikubwa nilichojifunza kwenye maisha ni kuanza na ulichonacho ili kufanya kinachowezekana kwa wakati huo. Kabla hujafanya yasiyowezekana unapaswa kuwa tayari kuanza kutumia kile ulichonacho kwanza.
Ukiwa Mwaminifu Kwenye Mambo Madogo Utaaminika Kwenye Makubwa Pia
Kwenye Biblia kuna mfano ambao unajieleza vizuri tu. mfano huu ni wa bwana mmoja ambaye alikuwa anataka kusafiri na kwenda safari ya mbali. Kabla ya kusafiri huyu bwana aligawa mali zake kwa watu watatu. Mmoja alimpa talanta tano, mwingine alimpa talanta mbili na mwingine akampa moja. Yule aliyekuwa na talanta tano na yule wa mbili walizizalisha vizuri tu na kuziongeza mara dufu yake, ila huyu wa talanta moja akawa ameichukua na kuizika. Mpaka bwana wake aliporudi ndipo jamaa akaanza kulalamika kwa kumwabia bwana wake kwamba, nilijua kuwa wewe unavuna usipopanda na maneno mengine…wenzake waliokuwa wametumia vizuri zile talanta, bwana wao alipokuja aliwasifia kwa kuwambia, vyema mtumishi mwenye haki, umekuwa mwaminifu kwenye mambo madogo utakuwa mwaminifu kwenye mambo makubwa pia.
Huwezi kuaminiwa fedha nyingi wakati kile kidogo ulichonacho kinakushinda kukitunza.
Najua kwamba watu wengi wanapenda kupata fedha nyingi za mtaji, ila wanashindwa kutumia zile kidogo walizonazo. Huwezi kuaminiwa na kupewa fedha nyingi wakati zile kidogo zinakushinda tu. anza kutumia vizuri kwanza zile fedha kidogo ulizonazo ili uweze kuaminiwa na kupewa fedha nyingi zaidi ya hizo hapo. kuwa mwaninifu kwenye mambo madogo kwanza kabla hujakabidhiwa mambo makubwa
Hata mtu au bashara ikienda kukopa benki huwa haipewi fedha zaidi ya vile inavyoweza kulipa. Kwa nini? kwa sababu,inapaswa kuonesha kwanza kile kile kiasi kidogo inaweza kutumia vizuri na kukikuza zaidi ya hapo. Maana kuna watu wakipata fedha zaidi ya vile wanavyostahili ni kama wanarukwa na akili zao. Kuwa mwaminifu kwanza kwenye mambo madogo, utakabidhiwa makubwa. anza kuwa mwaminifu kwa kile ulichonacho leo hii
Inawezekana jamaa aliyepewa talanta moja kwenye biblia alikuwa analalamika pia kuwa hana mtaji. Pengine kwa kuona wenzake waliopewa talanta tano kwa mbili, aliamua kususa kuitumia haya hiyo moja.
La leo hii ukiambiwa talanta moja ni sawa na shilingi ngapi, unaweza kuona kwamba huyu jamaa alikuwa amepewa mtaji mkubwa tu ambao hakuutumia. Nikwambie talanta moja ni sawa na shilingi ngapi?
Kadiri ya mtandao wa Wikipedia, kwa viwango vya sasa hivi, talanta moja ni sawa na dola milioni moja na laki nne. Ambazo ukiziweka kwenye fedha za Tanzania zinafika bilioni 2 na zaidi. kumbe huyu jamaa alipewa utajiri mkubwa sana, ila hakuutumia.
Ninachotaka kukwambia leo hii ni kwamba na wewe unao utajiri mkubwa sana, kuliko ambavyo unafirikia, kuna mitaji uliyonayo ila huitumii na sasa wacha tuanze kuiona…
N.B. Ili kuendelea kusoma mpaka mwisho, utapaswa kupata ebook hiyo hapo chini kwa shilingi elfu 2 tu badala ya shilingi elfu 3. Lipia kwa 0684408755 jina ni GODIUS RWEYONGEZA. Ukishalipia, utatumiwa ebook hiyo kwa whatsap.
Kupata eBook hii bonyeza hapo chini au wasiliana nami kwa 0755848391
Kama unataka kupata ebook kama hiyo bure kila mwishoni mwa wiki. Basi Bonyeza Hapa
6 responses to “MITAJI 8 ILIYOKUZUNGUKA NA JINSI YA KUITUMIA”
[…] Tayari nimeshaandika ebook inayoeleza mitaji 8 iliyokuzunguka na jinsi ambavyo unaweza kuitumia hiyo mitaji. […]
[…] SOMA ZAIDI: MITAJI 8 ILIYOKUZUNGUKA NA JINSI YA KUITUMIA […]
[…] Usiwaze. Mtaji wa wewe kuanza biashara unaweza kuupata tu kirahisj. Na tena tayari una MITAJI 8 ILIYOKUZUNGUKA na ambayo unaweza KUANZA KUTUMIA LEO. […]
[…] 70. soma kitabu changu cha MITAJI 8 ILIYOKUZUNGUKA NA JINSI YA KUITUMIA […]
[…] MITAJI 8 ILIYOKUZUNGUKA NA JINSI YA KUITUMIA […]
[…] usikubali kukaa ukiwa umetulia bila ya kufanya chochote. Kuwa kwenye mwendo mara zote. SOMA ZAIDI: MITAJI 8 ILIYOKUZUNGUKA NA JINSI YA KUITUMIANB: Ile ofa ile, ya idi ile ya mtu mmoja kujiunga na kozi yangu ya uandishi, imeshachukuliwa. Pole […]