Kuna tabia moja ya fedha ambayo ningependa uifahamu siku hii ya leo. Na tabiai hiii ni kwamba fedha huwa inawaendea zaidi wale wenye nazo na kuwakimbia wale ambao hawana. Kwa hiyo kama wewe una tabia ya kuwa unapokea fedha na kuitumia yote kwa mkupuo bila kubakiza kitu, unapaswa kufahamu kwamba fedha zitakuwa zinakukimbia mara kwa mara. Anza kujijengea nidhamu na kuwa unakaa na fedha hata bila kuitumia. Kwa kufanya hivi, unatoa nafasi ya fedha zaidi kuja kwako.
Je, mara yako ya mwisho kukaa na fedha kwa muda mrefu bila kuitumia ilikuwa ni lini?