Hiki Ndicho Kitu Kinachofanya Watu Wakuombe Fedha


Rafiki yangu bila shka umekuwa na siku bora sana. hivi umewahi kujiiuliza ni kwa nini ukiwa na fedh ndio watu wanajitokeza kukuomba fedha? Ila pale zikiisha tu watu wanaondoka mpaka pale utakapokuwa na fedha? Kuna kitu kimoja tu ambacho kinawafanya watu wakuombe fedha. Na kitu hiki ni kuwa wewe ukipokea fedha hautulii. Badala yake unakuwa unawashwa washwa. Sasa watu walio karibu yako wanakusoma na hivyo wanajisogeza kwako ili kukuomba fedha. Ila zikiisha wewe mwenyewe unakuwa mpole kiasi kwamba wanakusoma tena na hivyo wanaamua kuondoka maana unakuwa sio mtu wa msaada wowote tena kwao.

Kwa hiyo basi, kitu cha kufanya leo

1. hakikisha kwamba unakuwa na aina ile ile ya maisha bila kujali kwamba una fedha au la!

2. unapopokea fedha kuwa na utaratibu wakutulia kama vile fedha haijaingia walau kwa wiki moja. yaani, ndani ya kipindi hiki hapa unakuwa haujagusa hiyo fedha yako kwa ajili ya matumizi. Unakuwa unaendelea na maisha kama vile hakuna kilichotokea.

3. usitumie fedha yako hovyohovyo. Badala yake hakikisha kama unaenda kufanya unaandika vile ambavyo utanunua, na hakikisha unanunua hivyo tu.

4. itumie ile fedha ambayo ulikuwa unaitumia kwenye mambo ambayo hayana maana kuwekeza sehemu ambayo itakuletea fedha zaidi siku za mbeleni.

 

Rafiki yangu, kwa kufuata haya ambayo nimeakuandalia hapa, ni wazi kuwa unaenda kuepukana na tabia yako ya kuwa kama umeweuka pale unapopokea fedha kiasi cha kuwafanya marafiki wawako wawe wanakuja kwako kwa ajili ya kukuomba fedha na kukukimbia pale ambapo fedha yako inaisha.

Chukua hatua,

Nakutakia siku njema sana.

UMEKUWA NAMI,

GODIUS RWEYONGEZA

TUWASILIANE 0755848391

,

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X