Ni takribani wiki sasa tangu nimeandika andiko langu nikieleza kuwa kuamka asubuhi ni tabia. Katika makala hiyo nilieza jinsi ambavyo unaweza kujenga tabia ya kuamka asubuhi na mapema hata kama hukuwahi kujenga tabia hii hapo awali.
Hata hivyo, kuna mtu amejaribu kuufuata ushauri huo wa kuamaka asububuhi na mapema na umemshinda. Ameniambia kwamba ameweka alarm kama nilivyoshauri ili iweze kumwamusha asubuhi na mapema ila hiki kitu anaona kama vile hakifanyi kazi.
Binafsi kwanza nipende kumpongeza kwa uamuzi huo. Kama na wewe uliweka uamuzi huo wa kuhakikisha kwamba unaamaka asubuhi na mapema, hongera. Hata hivyo, kama bado hujaweza kuamka asubuhi na kama kila siku alarmikiiia wewe unaizima basi, ni wazi kuwa lazima kuna sehemu kuna tatizo. Hivyo, siku ya leo nimerudi ili uhakikisha kwamba naliondoa hilo tatizo mara moja na mwisho.
KWANZA, TATIZO HILI LINAANZIA KWENYE VIPAUMBELE. Naomba kujua wewe vipaumbele vyako ni vipi? Maana siku zote watu huwa wanaweka nguvu kule kwenye vipaumbele vyao. Kama mtu kipaumbele chake ni kulala basi atakipa nguvu hicho. Ndio maana kwa mfano, ukichukua shabiki wa Simba na Yanga utakuta kwamba kila sabiki anaisifia timu yake. Shabiki wa Simba ataisifia Simba, hata kama inayumba na shabiki wa Yanga ataisfia Yanga hata kama inayumba. Sasa na wewe hivyo, hivyo ukiona kwamba usingizi unaupa nguvu kuliko kuamka basi unapaswa kufahamu kuwa usingizi kwako ndio kipaumbele nambari moja huku vitu vingine vikiwa havina nafasi kubwa. kwa hiyo sasa ni wakati wako wa kubadilisha vipaumbele,
Siesemi kwamba usielale, hapana. Ulale tena masaa nane ukiweza. Ila unapofika muda wa kutoka ktandani,unakuwa umefika. Yaani, hapo hakuna kitu cha ziada isipokuwa tu kuhakikisha kwamba unakiacha kitanda ili uweze kuendelea na kazi nyingine zinazokusubiri
PILI, MALENGO YAKO. Ni vigumu kuamka asubuhi na mapema kama hauna malengo na kazi ya kufanya. Kwa hiyo sehemu ya kwanza unapopaswa kuanzia sio kwenye kuamka bali kwenye kuweka malengo. Sasa labda wewe nikuulize, malengo yako ni yapi? Unataka kwenda wapi? Kwa nini unataka kwenda huko? Unataka kwenda na nani? Unataka kufika baada ya muda gani? Malengo, malengo, malen go. Bila malengo rafikii yangu utaangamia na kama unalala sana, kiasi huwezi kujiuziua basi ni wazikuwa umeshaanza kuangamia.
TATU, UNAJIHOJI SANA. ujue muda wa kuamka unapofika, usingizi unaonekana ni mtamu sana. tena asikwambie mtu ule usingizi wakuanzia saa 10 alfajiri ni usingizi mzuri sana. Hivyo, kiasi kwamba ukifika muda kuamka bado unakuwa na unashawishika kwamba walau uendelee kulala dakika tano za ziada. Ukiongeza dakika tano zinakuwa kumi, kumi zinazaa saa moja. unakuja kustuka kwamba umeamka muda wako uleule wa siku zote. Unaishia tu kujiambia kwamba nitaamka mapema kesho na kesho yake hali hiyo hiyo inajirudia na hivyo kujikuta wamba kila siku unarudia mambo yaleyale na muda wako wa kuamka kila siku unakuwa ni ule ule.
Sasa ninachopendakukwambia ni kwamba; kiufupi unahitajhi kuwa kama katili kidogo juu yako. Yaani, wewe unapaswa kuwa dikteta wako mwenyewe. Ukifikia muda wa kuamka basi ni kuamka. Na kwa kuwa mpaka hapa utakuwa tayari umeweka malengo, kitakachofuata ni wewe kufanyia kazi malengo yak o hayo ambayo umeweka bila ya kuchelewa
SOMA ZAIDI; Usifanye kitu kikiwa cha kwanza unapoamka asubuhi
NNE, UNACHELEWA KULALA. Kama unachelewa kulala usitegemee kwamba utakuwa na ujasiri wa kuamka mapema. Ila ukilala mapema tusema saa mbili au saa tau, huwezi kushindwa kuamka mapema. Maana mwili wako unakuwa tayari umeshapitia kwenye mzunguko wote wa usingizi na na hivyo, kuwa tayari sasa kwa ajili ya kufanya kazi.
Ila hapa kuna kitu kinanifanya nijiulize, kinachokuchelewesha wewe kulala ni kitu gani? Je, hicho kitu kinakupelekea wewe kufaninisha malengo yako au ndio kwanza kabisa kinakukwamisha na kukufanya uendelee kurudi nyuma kila siku? Kama hakikusogezi kwenye malengo yako basi ni wazi hapo kuna tatizo. Kama unachelewa kulala eti kwa sababu unaangalia tamthilia , basi ni wazi kuwa kuna tatizo. Na ukweli ni kwamba kama ukiamka mapema, tuseme saa 11 asubuhi. Na ukaweka kazi inayostahili kuanzia muda huo. Ikifika saa tatu usiku ni wazi kuwa utakuwa tayari umechoka, na hapo utahita kuutuliza mwili wako ili kuuandaa kwa ajili ya kesho yako.
TANO; HAUPANGILIII SIKU YAKO KABLA YA KULALA
Hiki ni kitu kingine ambacho kinakufanya wewe hapo ukwame na kushindwa kuamka asubuhi na mapema. Kwa hiyo, unahitaji kuhakikisha kwamba unajenga utaratibu wa kuwa aunapangilia siku yako usiku mmoja kabla. Yaani, yale majukumu yako ya siku ambayo inafuata unapaswa kuhakikisha kwamba unayapangilia kabla ya kulala. Hivyo, ile unapoenda kulala akili yako na kila kitu kinakuwa kwenye kuamka mapema na unakuwa unajua kwamba kesho nikiamka ninapaswa kufanyia kazi haya majukumu. Nakwambia, ratiba zako zikiwa hivi ni wazi kuwa huwezi kushindwa kuamka asubuhi na mapema ili kuweza kuendelea na shughuli nyingizo.
Ila kama hauna majukumu ambayo umeyapganilia usiku mmmoja kabla, basi ni wazi kuwa utaona kuamka asubuhi na mapema kama kikwazo kwako.
Rafki yangu hivyo ndivyo vitu vitano ambavyo mpaka sasa hivi vinazidi kukukwamisha na kukufanya usiamke asubuhi na mapema. Unapaswa kuhakikisha kwamba unavifanyia kazi kuanzia leo hii ili uweze kupata matokeo mazuri haswa linapokuja suala zima la kuamka asubuhi na mapema. Napenda tu nikukumbushe usemi wa Benjamini Franlin ambao niliulelza kwa kina kwenye makala ya wiki iliyopita, kuwa kulala mapema na kuamka mapema kunamfanya mtu awe mwenye afya njema, tajiri na mwenye busara. Sasa sidhani kama wewe usingependa kupata vitu hivi vitu vyote kwa pamoja au hata na zaidi. Je, wewe umesubiri nini kuanza kuamka asubuhi na mapema? Chukua hatua sasa fanyia kazi haya yote ulyojifunza hapa ili uweze kupata matokeo mazuri.
Hata hivyo kabla sijakuachia kabisa siku ya leo ningependa nikuache kwa kukupa tahadhari. Kama nilivyokuandikia wiki iliyopita ni kwamba kuamka asubuhi na mapema ni tabia kama zilizyo tabia nyingine. Na siku zote tabia huwa hazijengwi kirahisi hasa kama ni tabia nzuri. Hivyo, kitu kikukbwa ambacho unapaswa kufahamu ni kwamba; tabia mpya huwa ni ngumu kujenga mwanzoni, tena huwa zinakuwa ngumu zaidi katikati ila baadaye tabia hizi huwa zinaonekana ni rahisi sana.
Kwa hiyo, na wewe katika kujenga tabia yako hii ya kuamka asubuhi na mapema unapaswa kufahamu kwamba , itakuwa ngumu kwako mwanzoni. Tena itakuwa ngumu zaidi katikati, ila baadaye itakuwa rahisi ukiendelea kuwa king’ang’anizi.
Kitu kingine ni kwamba tabia kama hii ya kuamka aubuhi na mapema haijegwi ndani ya siku moja kama ilivyokuwa kwa mji Roma. Inachukua muda wa kuanzia siku 66 na kuendelea. Sasa jipe muda na tabia hii ya kuamka mapema itakuwa ni sehemu ya pili ya maisha yako.
Umekuwa nami rafiki yako wa ukweli Godius Rweyongeza
Hakikisha Umesubscribe kwenye Channel yangu ya youtube kwa KUBONYEZA HAPA
Jiunge na mfumo wa kupokea makala maalumu kwa njia ya barua pepe kwa KUBONYEZA HAPA
Jipatie nakala za vitabu vyangu vya kiswahili kwa KUBONYEZA HAPA
Kama ungependa kujifunza kuhusu uandishi kutoka kwangu wasiliana nami kwa 0755848391
Kupata nakala ngumu ya kitabu cha KUTOKA SIFURI MPAKA KILELENI basi tuma ujumbe au piga kwa 0755848391
Kutengenezewa blogu yako kitalaamu tuwasiliane kwa 0755848391
kila la kheri
One response to “Sababu Tano Kwa Nini Unashindwa Kuamka Asubuhi Na Mapema Na Kitu Gan Unaweza Kufanya Sasa Hivi”
[…] SOMA ZAIDI: Sababu Tano Kwa Nini Unashindwa Kuamka Asubuhi Na Mapema Na Kitu Gan Unaweza Kufanya Sasa Hivi […]